Celina Mathew
Maalim Seif Sharif Hamad |
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif
Sharif Hamad ameutua mgogoro wa chama che kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima, Josephat Gwajima huku kiongozi huyo wa kidini akitangaza kuwa
atamlipua Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba Jumapili ijayo.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati alipomtembelea
Askofu Gwajima, Maalim Seif alibainisha kwamba amemweleza kiongozi huyo mambo
mbalimbali ikiwemo suala la mgogoro ndani ya CUF, aliodai umesababishwa na
Lipumba.
Alisema kuwa ameamua kwenda kwa Askofu Gwajima kumweleza
hayo kwa sababu ni rafiki yake na hawajaonana siku nyingi lakini pia kiongozi
huyo alikuwa haelewi mgogoro wa CUF umesababishwa na nani.
"Nimemweleza Askofu Gwajima mambo mengi hususani
mgogoro wa CUF hivyo ataamua mwenyewe nini afanye kutokana na
niliyomweleza,"alisema.
Aliongeza kuwa mbali na kwenda kwa Gwajima pia ameshazungumza na viongozi wengine wa
dini husuani ya Kiislamu.
Kwa upande wake, Askofu Gwajima alisema kuwa ameshafahamu
chanzo cha mgogoro huo kwa kuwa Maalim ni rafiki yake wa siku nyingi lakini
Lipumba hana urafiki naye.
Alipoulizwa kama watu watarajie chochote kutokea kuhusu
CUF, Maalim Seif na Lipumba kwenye ibada Jumapili ijayo, Gwajima alijibu:
“Kumbe mnajua, subirini Jumapili ifike nitamlipua na tutajua amekula maharage
ya wapi.”
0 comments:
Post a Comment