Venance Matinya, Mbeya
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini
na Nchi Kavu (Sumatra) imefanya mkutano na wadau wa usafirishaji mkoani Mbeya
wenye lengo la kupokea maoni ya kurekebisha na kuboresha kanuni
mbalimbali.
Akifungua mkutano huo uliofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa, Mwenyekiti wa Mkutano ambaye pia ni Mjumbe wa
Baraza la Taifa la Usalama barabarani, Henry Bantu alisema lengo ni
kushirikisha wadau kwenye mchakato huo.
Alisema kanuni zinazopitiwa ni pamoja na
kanuni za Leseni za usafiri wa magari ya abiria, 2017, Marekebisho ya kanuni za
leseni za usafirishaji wa pikipiki 2017 na Marekebisho ya kanuni za leseni za
usafirishaji wa Magari ya mizigo ya mwaka 2017.
Alisema sekta ya usafiri ni muhimu katika
Serikaliya awamu ya tano katika kuelekea kwenye Nchi ya Uchumi wa Viwanda hivyo
ili kupata mafanikio ni bora kuboresha sekta hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Sheria Sumatra
makao makuu, Leticia Mutaki alisema lengo la maboresho ya kanuni hizo ni
kuhakikisha usafiri wa barabara unakuwa bora na salama, viwango vya adhabu
vilivyopo vinaendana na wakati na kuendana na mabadiliko ya usafiri wa
barabara.
Alitaja malengo mengine kuwa ni kuendana
na mikataba ya kimataifa pamoja na kuongezeka kwa huduma za usafiri mbalimbali
ambazo zilikuwa hazimo kwenye kanuni.
Kwa upande wake mmoja wa Wadau wa
Usafiri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri
(CCC)Sumatra Mkoa wa Mbeya, Said Mohamed
alisema tatizo sio mapungufu ya Kanuni bali ni changamoto ya usimamizi kutoka
Sumamtra.
Alisema mara nyingi abiria hupoteza
mizigo kwenye magari lakini hakuna hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na
ukaguzi wa tiketi ambazo haziendani na kanuni za usafirishaji kwani baadhi
huandika mizigo sio dhamana ya msafirishaji.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni
ubovu wa magari yanayopewa leseni ya kusafirisha abiria kutokana na muundo wa
ukaguzi ambao hufanywa na Polisi lakini Sumatra anatakiwa kutoa kibali
bila kujiridhisha.
0 comments:
Post a Comment