Joyce Kasiki, Dodoma
Shaban Shekilindi |
MBUNGE wa
Lushoto Shaban Shekilindi (CCM) ameihoji Serikali lini itajenga Chuo cha Ufundi
stadi cha Veta wilayani Lushoto ili kutimiza ahadi yake ilivyoahidi kujenga
vyuo hivyo katika kila wilaya kwa leongo la kuwasaidia Vijana nchini
kujifunza stadi za kazi mbalimbali .
Akiuliza swali
Bungeni jana,Shekilindi alisema,ujenzi wa Chuo katika wilaya ya Lushoto na Nchi
nzima kwa ujumla ,utasaidia Vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
utegemezi.
"Je,lini
Chuo cha Veta kitajengwa katima wilaya ya Lushoto?" alihoji Shekilindi
Akijibu swali
hilo,Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stellah Manyanya
alisema,Serikali itaanza ujenzi katika wilaya ya Lushoto mara baada ya kukamilisha
miradi ya you ya Veta iliyoanzishwa katika vyuo vya Lidewa,Namtumbo,Chunya na
Ukerewe.
Hata hivyo
alisema,wakati juhudi mbalimbali zinaendelea za kutafuta fedha na ufadhili wa
kujenga vyuo,Serikali inashauri wananchi wa wilaya ya Lushoto waendelee kutumia
Chuo cha Veta cha Mkoa wa Tanga na vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Muheza na
Handeni na vyuo vingine vilivyosajiliwa na Mamlaka ya Veta nchini.
Katika swali
lake la nyongeza Mbunge huyo alitaka kujua kama Serikali haioni
kuchelewa
kujenga Chuo hicho wilayani Lushoto ,italimbikiza Vijana wengi watakaoikosa
elimu ya veta pia alitaka kujua Kama Waziri yupo tayari kwenda kuwaona baadhi
ya majengo yaliyopo wilayani humo ambayo hayatumiki Kama yanaweza kutumika kwa
ajili ya kutoa mafunzo ya veta.
Akijibu Mhandisi
Manyanya alisema,Serikali haina Lengo la kudidimiza maendeleo ya wilaya ya
Lushoto kwa Vijana kukosa elimu ya Veta huku akisema,bado Serikali inaendelea
kutafuta fedha na kwamba wakati muafaka ukifika na fedha
zitakapopatikana,Serikali itajenga Chuo hicho.
Aidha
alisema,ataenda wilayani Lushoto kuwaona majengo hayo na kama ataona
yanafaa,Setikali itayatumia kwa ajili ya kuanzisha Chuo cha Veta.
Alitumia fursa
hiyo kuiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano kupeleka msaada wa haraka ili kurejesha mawasiliano ya barabara ya
Lushoto-Dar es Salaam kufuatia kubomoka kwa madaraja katika barabara hiyo.
Shekilindi
alitoa kauli hiyo Bungeni mjini hapa jana wakati alipokuwa akiuliza swali la
nyongeza ambapo alisema, mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Lushoto mkoani
Tanga zimeleta madhara na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano katika
barabara ya Lushoto-Dae Es Salaam, Lushoto-Arusha na Lushoto-Tanga jambo ambalo
limeathiri uchumi wa wakazi wa wilaya hiyo.
Alisema mvua
hizo zimesababisha madaraja kukatika na kwamba zaidi ya kilometa 32 katika
barabara hiyo hazina mawasiliano,huku akisema msaada huo utasaidia
kunusuru maisha ya wananchi wa Lushoto na uchumi unaotegemea barabara hiyo.
“Mheshimiwa
naibu spika kwa kuwa jambo hilo ni kubwa na limeathiri uchumi wa wakazi wa
Lushoto niambe serikali ipeleke msaada wa haraka, pia nitoe pole kwa wananchi
wa jimbo la Lushoto na wilaya ya Lushoto kwa ujumla,”alisema.
Shekilindi
alibainisha kuwa, tarayi alikwisha zungumza na Menea wa Wakala wa
Barabara(TANROAD), mkoa wa Tanga ambaye aliahidi kushugulikia jambo hilo,
anaamini kuwa litashughulikiwa haraka.
0 comments:
Post a Comment