Mery Kitosio, Arusha
Mrisho Gambo |
MAJERUHI wa ajali ya gari iliyohusisha vifo 35 vya wanafunzi, walimu
pamoja na dereva wa shule ya msingi Luck Vicent
wilayani Karatu, wamesafirishwa jana kwenda Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi .
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa
Kia, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa majeruhi hao
wanasafirishwa na ndege ya Shirika la Samaritan Purse ili kuwawezesha kupatiwa
huduma za matibabu zaidi ambazo zitaweza kurejeshea afya zao.
Gambo alisema kuwa Serikali imejitahidi
kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wamewafariji
wale wote waliofikwa na msiba na hata kuhakikisha kuwa majeruhi waliobaki
wanapatiwa huduma ambazo zitaweza kunusuru maisha yao.
Gambo aliwataka wakazi wa jiji la Arusha
na viunga vyake kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwa inakwamisha
huduma za kijamii kwa ajili ya kuchanganya na shuguli za kisiasa.
"Naombeni sana wana Arusha muache
kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwani hii mitandao imepotosha sana mambo
mengi imehusisha huduma za kijamii kuwa mambo ya kisiasa hali ambayo
inasababisha hata wanaojitokeza kuchangia maafa haya kuvunjika moyo kwa ajili
ya mambo yaliyoandikwa kwenye mitandao ya hiyo"-alisema Gambo
Alidai kuwa huduma za kijamii hazipaswi
kuhusishwa na shughuli za kisiasa kwani endapo zitahusishwa zitakwamisha hata
wale wanaoendelea kufariji kushindwa kuendelea na moyo huo.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro
Nyalandu ambaye ni mmoja wa waliojitolea kufanikisha safari hiyo aliwataka Watanzania
kuendelea kuombea majeruhi hao ili wapone haraka.
Safari ya majeruhi hao kuelekea Marekani
saa 5:40 asubuhi wakiambatana na mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Gaspa ambaye
amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki.
0 comments:
Post a Comment