Mwandishi Wetu
Dk. Charles Tizeba |
WAZIRI wa Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles
Tizeba, amesema kilimo kina mchango mkubwa katika kufanikisha azma ya Serikali
ya kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa kati na viwanda.
“Kilimo hakiepukiki katika dhamira ya Serikali kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwani malighafi nyingi zitatokana na mazao ya
kilimo,” alisema Waziri Tizeba katika Mkutano wa Kumi wa Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Dk. Tizeba aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba Tanzania
ya viwanda inawezekana na kushauri uwekezaji mkubwa ufanyike pia kwenye kilimo.
“Tumefanya maboresho makubwa katika sekta ya kilimo
ilikuendana sambambana azma ya serikali ya viwanda. Kwa mfano tumetoa tozo
mbalimbali ili kuchochea uzalishaji,” alisema.
Dk. Tizeba alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk.
Magufuli imechukua hatua mbalimbali madhubuti kuhakikisha kuwa pembejeo za
kilimo ikiwemo mbolea inashuka na kumpa nafuu mkulima.
“Bei ya mbolea ni ghali sana na sasa tumeangalia mnyororo
wa upatikanaji wake,” alisema.
Alieleza kwamba jitihada za makusudi zimeshachukuliwa
kuhakikisha bei ya mbolea na pembejeo nyingine za kilimo zinashuka na kutoa
nafuu kwa mkulima.
Kwa mujibu wa Dk. Tizeba, tafiti nyingi zinaonyesha kuwa
kutangaza zabuni ya kuagiza mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement) kutasaidia
kushusha bei ya mbolea nchini na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.
“Tumeandaa pia utaratibu wa utunzaji wa mazao ya msimu
ilikuyaongezea thamani staili mazao hayo,” alisema.
Waziri Tizeba alisema kumekuwa na upotevu wa asilimia 48
ya mazao yote yanayovunwa hapa nchini na wizara yake inaangalia namna ya kuzuia
upotevu huo.
Kwa upande wa mbegu Tizeba alisema mbegu zinazozalishwa
hapa nchini zimekuwa ghali sana ukilinganisha na zile zinazotoka nje.
“Utashaanga mbegu kwa mfano zinazoingizwa toka nje
zitaunza 1,500 kwa kilo lakini za hapa ndani zitauzwa 7,000, lakini pia mbegu
hizo hazitoshi wala kuwafikia wakulima wote kwa wakati,” alisema.
Alibainisha kwamba Serikali imeshapitia na kupitisha
kanuni zitakazotumika kupitisha mbegu ambazo zitakazokuwa zinatumika ambapo
hapo awali ilikuwa inachukua miaka mitatu na sasa itakuwa ni mwaka mmoja tu.
Mkutano huo wa Baraza ambao ulishirikisha sekta za umma
na biashara ulibeba maudhui ya Tanzania ya Viwanda; Ushiriki wa Sekta Binafsi
ambapo uliongozwa na mwenyekiti wake Rais John Magufuli.
0 comments:
Post a Comment