Shaban Njia, Kahama
Matomora Michael |
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Ushetu
Wilayani hapa, Matomora Michael, amesema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika (KACU),
wametishia kutotoa ushuru wa asilimia tano kwa halmashauri hiyo kwa kile
kinachadaiwa kuwa fedha hiyo hairudi katika maeneo ya wakulima wa tumbaku kwa
ajili kutengeneza miundombinu ya barabara.
Matomora aliyasema hayo juzi katika
kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika kata ya Nyamilangano
ambapo alisema kuwa kitendo cha chama cha ushirika kutishia kutoa ushuru wa zao
la tumbaku ni kwenye kinyume na makubaliano ya ulipwaji kodi serikalini.
Alisema usemi huo ni upotoshaji kwa
wakulima wazao la Tumbaku ambalo ushuru wao mkubwa ndio inaotegemewa na
Halmashauri hiyo kama mapato ya ndani na kuongeza kuwa barabara hizo
tayari zimtengenezwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo makubwa ambayo
kimsingi ndio yanayolima zao la Tumbaku kwa kiasi kikubwa.
Aidhaa alisema ushuru kwa Halmashauri
hiyo sio kwa ajili ya kutengeneza barabara tuu na kuongeza unaweza kutumika
katika mambo mengine ya msingi yenye maslahi na Halmashauri hiyo ili
kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana na Wananchi wanapata huduma
zinazotakiwa za kijamii.
“Fedha hizo zinazotolewa na Chama kikuu
cha Ushirika Wilayani Kahama sio kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya
Barabara tuu katika Halmashauri yetu bali zinaweza kutumika katika kufanya kazi
zingine zenye maslahi na Halmashauri yetu ili kuwaletea wananchi maendeleo
katika eneo husik”, Alsema Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Ushetu.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya
Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga juzi ililaani vikali na kukanusha rasmi
kuhusi kitendo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli kutangaza
katika Vyombo ya habari kuwa ametoa msaada wa ujenzi wa barabara ipatayao mitaa
200 katika eneo la Kata Bulungwa Wilayani hapa
Akiongea katika kika kikao cha baraza
Madiwani juzi kiklichakaa katika makao makuu ya Halmashauri ya Ushetu
Nyamilangano, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Matomora Michael alisema kuwa
kitendo alichokisema Mbunge huyo katika vyombo vya habari ni kujitafutia
umaarufu wa kisiasa.
Alisema Kuwa Halmashauri yake ya Ushetu
ina kila kumbukumbu ya Mtui yryote ambaye anakuwa akitoa msaada na kuongeza
kuwa katika ofisi yake hajaona faili lololeau taarifa inayisema Mbunge huyo
ametoa msaada wa kujenga barabra katika kata ya Bulungwa ya kiasi cha mita
200.
“Mimi ninashangaa kwa James Lembeli
lusema kuwa ametoa msaada wa ujezi wa barabara ya mita 200 katika eneo amblo
lipo kariu na mahali anapoishi huku kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge wa
Jimbo la Kahama Mjini hajawahi kujenga hata kilometa moja leo hayupo katika
wadhifa huo atawezaje kujenga”, Alisema Matomora
Aliendelea kusema kuwa kauli hizo
zinaotolewa na Lembeli ni katika hali ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa
na kuongeza barabara hiyo ambayo inatoka katika kata ya Bulungwa kwenda katika
Vijiji vya Karo na Nyankende wananchi ndio walitoa mafuta kwa ajili ya
utengenezwaji wa kipande hicho na kuongeza lembeli yeye alishirikishwa kama
mkazi wa eneo hilo.
“Sisi kama Halmashauri ya Ushetu
tunashangaa Mungunge huyo aliyeongoza jimbo hilo hilo liliokuwa Kahama Mjini
hapo awali kuwa barabara ya kilometa tisa yeye anatafuta
umaarufu kwa mita 200 tuu huku Halmashauri yetu ikiwa haina kumbukumbu
yeyote ya mtu ambaye anaamua kujitilea kufanya jambo fulani lamaenedeleo katika
eneo husika”, Aliongeza Matomora.
0 comments:
Post a Comment