Joyce Kasiki, Dodoma
Boniventura Kiswaga |
MBUNGE wa Magu
Boniventura Kiswaga (CCM) amesema, Serikali inapaswa kutafakari upya ili
wanafunzi wanaochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na cha sita wapate elimu
hiyo bure .
Kiswaga alitoa
kauli hiyo Bungeni jana wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo alisema,Vijana
wengi wanaochaguliwa kuendelea na masomo hayo ,wanashindwa kuendelea nayo
kutokana na kukosa uwezo wa kifedha.
"Hivi sasa
tunakabiliwa na uhaba wa wataalam wa sayansi nchini,na hawa wanafunzi
wanaochaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita wengi
wanakuwa wamefaulu masomo ya sayansi na wanakosa uwezo wa kuendelea na masomo
hayo kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo,Serikali haioni kwamba
inapoteza wataalam,
"Na
je,Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka kulet bajeti Bungeni ili wanafunzi
hawa wasome bure?"
Awali katika
swali la msingi Mbunge hutonalitaka mpango wa Serikali wa kutoa elimu
bure kwa wanafunzi we kidato cha tano na cha sita.
Akijibu
,Manyanya alisema,kwa sasa Serikali haina mpango wa kutoa elimu bila malipo kwa
wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita .
"Badala
yake imejikita zaidi katika kuboresha miundombinu ambayo ni pamoja na
upungufu wa vyumba vya madarasa ,matundu ya vyoo,majengo ya utawala
pamoja na kumalizia changamoto za uhaba wa walimu wa sayansi na vifaa vya
kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na masuala ya Tehama.
Mhandisi
Manyanya alisema,kukamilika kwa miundombinu hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa wanafunzi
wote wenye sifa ya kuingia kidato cha tano wanapata fursa ya kuendelea na
masomo yao.
0 comments:
Post a Comment