Leonce Zimbandu
Simon Sirro |
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam, Simon Sirro, ametoa amri ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani Lazaro
Mbise kwa kosa la kuibiwa bastola na mtoto wake Lewis Lazaro ambaye ni mwanafunzi
wa chuo Kikuu cha St.Joseph.
Tukio hilo limetokea Mei 4, mwaka huu maeneo
ya Mbezi magari saba baada ya Jeshi la polisi kufanikiwa kumkamatwa kijana huo
na kukiri baada ya mahojiano.
Kamanda Sirro aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na kubainisha kuwa
mtuhumiwa alikiri kuwa bastola hiyo aliiba nyumbani kwa mzazi wake.
Alisema pia, pamoja na bastola hiyo
aliiba Sh. 800,000.
Alisema upelelezi unaendelea ili kujua
lengo la mtuhumiwa huyo kuiba silaha hiyo ya baba yake na kufahamu iwapo kama
kuna taarifa ya kupotea kwa silaha.
“Huu ni uzembe wa kushindwa kutunza
silaha, hivyo mzazi huyo anapaswa kuchukuliwa hatua, ikiwamo kukamatwa na
kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo,” alisema.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi
limewakamata watuhumiwa watatu kwa kosa la kuvujisha mtihani wa kidato cha sita
somo la kemia katika shule ya sekondari Chang’ombe.
Kamanda Sirro alisema kuwa polisi
walipokea siku kutoka kwa afisa wa Baraza la Mitihani Aron Mweteni kuwa Mei 5,
mwaka huu katika shule hiyo alimkuta mwalimu Mussa Elius akiingia darasani
akiwa na mwanafunzi Ritha Mosha.
Alisema Ritha alikuwa ndiye mtahiniwa wa
mtihani wa kidato cha sita unaoendelea akiwa na karatasi ya yenye maswali na
majibu ya somo la kemia.
“Baada kufuatilia ilibaini swali hilo ni
miongoni mwa mwasawali mtihani huo, hivyo watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa,
akiwamo Mwalimu Innocent Mrutu,” alisema.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo
limefanikiwa kukamata vipande sita vya meno ya tembo ambavyo thamani yake bado
haijafahamika hadi upelelezi utakapokamilika.
Tukio hilo limetokea katika maeneo ya
Chanika, Zingiziwa na kufanikiwa watuhumiwa wawili ambao ni Senei Abas mkazi wa
Buguruni na Juma Kong’owa fundi ujenzi mkazi wa Gongo la Mboto.
0 comments:
Post a Comment