Joyce Kasiki, Dodoma
HALMASHAURI ya
Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Serikali
za Mitaa (LAPF) imeanzisha kampuni ya ubia ya Mzizima Propeties Limited ambayo itaendesha
na kusimamia shughuli za kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo kila siku.
Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jafo alitoa kauli hiyo jana bungeni akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, Said
Kubenea (Chadema) ambaye alitaka kujua hatua zilizofikiwa na Serikali katika
kutekeleza ahadi ya kuhamisha kituo hicho cha mabasi.
Pia alitaka
kujua mradi wa kuhamisha kituo hicho utatumia kiasi gani cha fedha.
“Serikali iliahidi
kuhamisha kituo cha mabasi cha Ubungo na kukipeleka eneo la Mbezi jimbo
la Kibamba, lakini mpaka sasa jambo hilo halijatekelezwa, je
Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza ahadi hiyo, na je mradi huo
unatarajia kutumia kiasi gani cha fedha?” Alihoji Kubenea.
Akijibu swali hilo,
Jafo alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na LAPF wameanzisha
kampuni ya ubia itakayohusika na usimamizi na uendeshaji wa kituo hicho kila
siku.
Alisema kazi
inayoendelea ni kumtafuta mtaalamu mshauri kwa ajili ya kuthibitisha usanifu wa
mwisho na wa kina wa mradi ili kumpata mkandarasi wa ujenzi.
Alisema gharama
za ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi cha Mbezi Luis zimekadiriwa kuwa Sh bilioni
28.71 zitakazotolewa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Jiji na LAPF.
0 comments:
Post a Comment