Dalila Sharif
DIWANI wa
Makangarawe, Temeke, Idd Mahuta, amewataka abiria wanaosimama katika vituo vya
mabasi kusubiri usafiri, kuwa makini na mizigo yao ili kuepuka kuporwa na
vibaka wa maeneo hayo.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, alisema abiria huporwa mizigo na simu za mkononi
wanaposimama kituoni hapo, huku wengine wakiporwa kupitia madirishani wakiwa kwenye
daladala.
“Suala
la uporaji limeibuka kwa kasi hasa kwa abiria usiku wanaporudi kutoka kwenye mihangaiko
yao ya kila siku. Hali hii si nzuri, kwa sababu hutishia usalama wa wakazi
wangu,” alisema Mahuta.
Alisema
ni vema wakazi na abiria kuwa makini kuzuia uporaji unaojitokeza na kwamba
Polisi Jamii wako pamoja katika kulinda eneo hilo kwa kushirikiana na polisi wa kata
hiyo.
“Kwa
sasa kata yetu iko makini na tunamshukuru Mkuu wa Wilaya, Felix Lyaniva kwa
kutuongeza askari wanaotembea kulinda usalama wa maeneo hayo nina imani hata
matukio ya uporaji yatapungua,” alisema Mahuta.
Aliwataka
wakazi kuwa na ushirikiano na kutoa taarifa haraka tatizo linapotokea ili kulifanyia
kazi, pia kuhusu suala la usafi aliwashukuru wakazi wake kwa kuwa na umoja katika
kutunza mazingira.
0 comments:
Post a Comment