Joyce Kasiki, Dodoma
Zitto Kabwe |
MBUNGE wa Kigoma
Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) ametishia kurudisha shahada aliyonayo
kwa mwalimu wake, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara
na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, iwapo mwalimu huyo atashindwa kuisimamia
vizuri wizara hiyo.
Akichangia
katika hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 ya Zitto
alisema ana imani Profesa Mkenda ataitendea haki wizara hiyo.
“Mheshimiwa
Waziri, Katibu Mkuu wako ni mwalimu wangu wa uchumi, mwaka wa tatu ameniundisha
sekta zote za uchumi yaani unachukua unatafuta njia hii na njia hii ukiingiza
unapata kila kitu. Mimi sitaki kumwambia nimrudishie Digrii yake kwa sababu kwa
sasa yeye ndio Katibu Mkuu katika wizara hivyo anawajibika,” alisema.
Zitto ameitaka
Serikali kuhakikisha inafanya kila jitihada katika kuendeleza zao la katani akisema: "Hivi Mheshimiwa Mwijage mnakaa
katika ‘Cabinet’ mnajadili hii mipango kwa sababu mkikaa lazima kuna mtu
atasema mimi kuna miradi yangu,lakini tunajenga mabehewa,mabehewa yana
viti ,hivi mmefikiria namna gani ya kuendeleza zao la katani.’’
Aliongeza:
"Leo tunakutana baada ya mwaka mmoja ukichukua Mwezi Marchi 2016 na Mwezi
Marchi 2017 bidhaa za Viwanda ambazo tunauza nje zimeshuka kwa dola za
Kimarekani milioni 500 kutoka 1.4 mpaka 0.9 milioni dola sasa. Tunaposimama
hapa na kusema kazi inafanyika ,Waziri atusaidie kwamba iwapo kazi inafanyika
na kuna ongezeko la uzalishaji ni kwanini mauzo yetu nje yamepungua kwa kiwango
kikubwa.’’
Alisema,mambo
hayo wabunge wanapaswa kuyazingatia kwa sababu bidhaa za viwanda
zinazouzwa nje zinapopungua ,ni kwamba Viwanda vyetu vya ndani vimepunguza
uzalishaji maana kuna watu wamepoteza kazi maana kuna mapato ya serikali
yanapotea’’ alisema
Zitto alisema,
ndani ya miezi 12 ,Tanzania imepoteza mauzo nje kwa dola milioni 500
ambapo alidai ifikapo mwaka 2020 inawezekana kabisa kusiwe na hata
senti moja kutokana na mauzo ya nje.
Alisema,
Tanzania ina tatizo kubwa la kulinda viwanda vya ndani ambapo alidai Waziri wa
Wizara hiyo ni shahidi juu ya malalamiko anayopelekewa kila mwisho wa mwezi ya
watu ambao wanaingiz nguo kinyemela nchini.
‘’Wanaingiza
mafuta ya kula kinyemela katika nchi yetu,wanaingiza Betri zinakuwa za bei
ndogo na matokeo yake ni kwamba Viwanda vya ndani vinashindwa kushindana nao
katika soko’’
Alihoji ,takwimu
za kiwango gani cha betri Tanzania imeagiza kutoka China miezi sita ya kwanza
ya mwaka 2016 kwani ukienda Idara ya wateja ya China utakuta kwamba, kati ya
Januari mpaka Septemba mwaka jana Tanzania imeingiza Betri za China zenye
thamani ya Dola za Kimarekani 36.5.
"Ukija
kuangalia kwa Idara yetu ya Forodha hapa nchini betri ambazo zimeingia nchini
na ukalinganisha na TBS betri ambazo wamezifanyia ukaguzi kuwa ngapi zimeingia
nchini ni za dola Kimarekani milioni 5.3 maana yake ni kwamba kuna betri nyingi
sana ambazo zinaingia nchini hazipiti katika njia ya kawaida’’
Alisema Viwanda
ambavyo vinazalisha betri hapa nchini kama Panasonic ambavyo vimeajiri watu
vitakuwa vinashindwa kushindana na vile vya China.
"Tafsiri
yake ni kwamba tutaongea humu kuhusu viwanda na haya ni mambo ambayo
tunategemea kuona Waziri ukihangaika nayo kwa sababu Wahenga wanasema bora
ndege ambaye unayemkononi kuliko ambaye yupo juu ya Mti
"Tuna mradi
wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 7 katika reli,reli material yake sehemu
kubwa ni chuma unahitaji tani 50 za Chuma cha pua kujenga Kilomita moja ya reli
sio kwamba hatuna chuma tunacho Mchuchuma na Liganga’’
Alisema,kabla ya
kuanza kufikiria kutandika hayo machuma ya reli ilitakiwa Serikali iwe
imeshajenga uwezo wa kuzalisha kule ili fedha zote zibaki kule na ndani
ya nchi .
Aidha, Zitto
ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo ,aliitaka Wizara hiyo
kushughulikia miradi inayotengeneza ajira za ndani ambazo zingesaidia kwa kiasi
kikubwa kuchochea ukuaji wa sekta ya Viwanda huku akitolea mfano wa reli.
0 comments:
Post a Comment