Joyce Kasiki, Dodoma
Abdallah Bulembo |
MBUNGE wa kuteuliwa
Abdallah Bulembo (CCM) ameitaka Serikali kuyafungia maduka yote yanayouza nyavu
bandia, badala ya kuwachukulia hatua wavuvi wanaotumia nyavu hizo katika shughuli
za uvuvi.
Bulembo alitoa
kauli hiyo jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza. Alisema wavuvi
wanaotumia nyavu hizo za matundu madogo wamekuwa wakichukuliwa hatua mbalimbali
ikiwemo kuchomewa nyavu zao huku maduka yanayouza nyavu hizo yakiendelea kutoa
huduma.
"Je, ni
lini Serikali itayafunga maduka hayo yanayouza nyavu feki na kuwasababishia
wavuvi hasara?" alihoji Bulembo
Akijibu swali
hilo,Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba alisema katika
kupambana na uvuvi haramu imekuwa ikiwachukulia hatua watu wote wanaohusika
katika kusababisha uvuvi haramu wakiwemo wauzaji, watunzaji na wazalishaji wa
nyavu hizo, huku akieleza kuwa wakati mwingine wamekuwa wakifunga viwanda
vinavyobainika kuzalisha nyavu hizo.
Awali, katika
swali la msingi, Mbunge wa viti maalumu Maria Kangoye (CCM) alitaka kujua ni
lini Serikali itaimarisha huduma za ugani kwa kutoa mafunzo kwa kuongeza
udahili wa maafisa ugani kutoka 1,200 hadi 2,500 kwa lengo la kuwa na maafisa
ugani wengi na kuimarisha huduma za uvuvi na ufugaji samaki.
Pia alitaka
kujua kama kuna mkakati wowote wa Serikali wa kuzishirikisha halmashauri nyingi
katika mkakati wa kuhamasisha uchimbaji wa mabwawa na ufugaji wa samaki hasa
katika maeneo yenye ukame ili kuongeza lishe bora na ajira kwa vijana.
Akijibu swali
hilo, DkTizeba alisema,mkakati wa kuongeza udahili ili kuongeza Maafisa ugani
wa uvuvi,ulianza kwa wizara kuimarisha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi
(Feta) Katima Kampasi zake za Mbegani,Nyegezi,Kibirizi,na Mwanza.
Vile vile
alisema ili kuongeza udahili na wanafunzi,Setikali itakamilisha ujenzi wa
Kampasi za Mkindani (Mtwara) na Gabimori (Rorya) ifikapo mwaka 2019 ambapo kwa
ujumla vyuo vyote vitadahili wanafunzi 2,000 kwa mwaka ikilinganishwa na 1,200
wanaodahiliwa hivi sasa kwa mwaka.
Dk.Tizeba
alisema,vyuo hivyo vinzalisha wataalam wa uvuvi katika ngazi ya Astashahada na
Stashahada ambao hupata ajira Serikalini ,sekta binafsi na wengine hujiajiri
wenyewe.
Kuhusu mkakati
wa kuzishirikisha Halmashauri katika uchimbaji wa mabwawa alisema,wizara
kwakushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa imechimba visima virefu 101 kwa
ajili ya kujaza maji kwenye mabwawa ya kufugia samaki na malambo 1,381 kwa
ajili ya kunyweshea mifugo ambayo pia hupandikizwa samaki.
0 comments:
Post a Comment