Hussein Ndubikile
Rais Magufuli |
RAIS John Magufuli leo anatarajia
kupokea taarifa ya Kamati Maalumu ya Kuchunguza Mchanga mchanga wenye madini.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya
wajumbe wanane aliyoiunda Machi kumaliza
kazi yake.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Profesa
Abdulkarim Mruma, Profesa Justianian Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk
Yusuf Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery
Gombela.
Kamati hiyo iliongozwa na Profesa Mruma
ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) chini ya
Wizara ya Nishati na Madini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa tukio la upokeaji
taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku likitarajiwa kurushwa
moja kwa moja na vyombo vya habari na tovuti rasmi ya Ikulu.
Msigwa alisema matangazo ya kupokea
taarifa hiyo yataanza kurushwa mbashara kuanzia saa 3:30 asubuhi kutoka Ikulu
huku ikiwasisitiza wananchi kutazama na kusikiliza.
0 comments:
Post a Comment