Joyce Kasiki, Dodoma
Ummy Mwalimu |
SERIKALI imesema
asilimia 60 ya Watanzania wanategemea tiba inayotolewa na waganga wa tiba asilia.
Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo jana
wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (CCM)
aliyeihoji Serikali kwa nini haitambui mchango wa waganga hao na ikawapa elimu
ya masuala ya afya.
"Hivi siku
zote watu wamekuwa wakiwasemea wasanii kwamba wanatumika wakati wa uchaguzi na
baada ya hapo wanasahaulika,lakini kwa kipawa nilichonacho na nikiangalia humu
ndani (Bungeni) ,wabunge wote mnaonekana mmepita kwa waganga hawa
kama hawapo labda wawili au watatu,kwani Serikali haitoi elimu kwa kundi hili
ambalo limekuwa kimbilio la watanzania?" alihoji Kasheku
Akijibu swali
hilo, Ummy alisema Serikali inatambua mchango wa watu hao kwa kuwa kundi kubwa
linawategemea waganga hao wa tiba mbadala.
Mapema katika
swal la msingi Mbunge wa Ushetu Elias Kwandikwa (CCM) alitaka kujua ni waganga
wangapi wa kienyeji wamekamatwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kufuatia
msako ambao umekuwa ukifanywa na jeshi hilo.
Akijibu, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuf Masauni alisema,waganga wa kienyeji
waliokamatwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ni 26 na kushitakiwa
kutokana na kufanya biashara ya uganga bila kibali na kupatikana na
nyara za Serikali.
"Katika
kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya waganga 16 walikamatwa na kufikishwa
mahakamani ,Kati ya hao waganga saba walipatokana na hatia kwa kufungwa miaka
miwili kila mmoja au kulipa faini ." alisema Masauni
Alisema,jumla ya
watuhumiwa sita katika kesi tofauti walilima faini ya jumla sh.milioni
1.25, mtuhumiwa wa kesi moja alihukumiwa miaka miwili bila yeye kuwepo
mahakamani ambapo juhudi za kumsaka zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment