Mery Kitosio na Wankyo Gati, Arusha
Mrisho Gambo |
TAASISI za Eco valley advisers, Clouds
media pamoja na Time tickets, wamekabidhi kwa uongozi wa mkoa wa Arusha Sh
4,444,0331, ikiwa ni rambirambi zilizochangwa na Watanzania kupitia mfumo wa
harambee wa kusaidia janga la ajali lililotokea katika shule ya luck vicent.
Rambirambi hiyo ilikabidhiwa jana kwa
mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kushuhudia na uongozi wa shule hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, mshauri
elekezi wa Time ticket Avit Buchwa alisema kuwa taasisi hizo zilikubali kwa
pamoja kuunganisha nguvu katika kusaidia kwa hali na mali pindi mtu au kikundi kinapopata
majanga.
Alisema kuwa ndani ya kipindi kifupi
kichozidi siku nne wachangiaji wapatao 721 waliweza kuchangia kiasi hicho cha
fedha.
Akizungumza kwa niaba ya wafiwa na
wakazi wa Arusha, mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo alisema kuwa amefarijika sana
kuona Watanzania wakiwa wamoja katika kipindi hiki cha majonzi.
Gambo alisema kuwa ni jambo la kutia
moyo na kujivunia kwamba sasa upo mfumo wa harambee wa tehama ambao unaweza
kukusanya michango kwa ufanisi na uwazi.
0 comments:
Post a Comment