Joyce Kasiki, Dodoma
OFISI ya Spika
na Bunge la Jamhuri ya Muungano limetoa Sh milioni 100 kutoka posho za wabunge
kwa ajili ya rambirambi kwa wazazi wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya
Lucky Vincent ya Arusha waliopoteza maisha.
Wanafunzi hao
walipoteza maisha Mei 6 wakati wakitoka Arusha kwenda Ngorongoro kufanya
mtihani wa ujirani mwema kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya darasa la saba.
Mapema kabla ya
kikao cha Bunge kuanza, Spika Job Ndugai aliwaongoza wabunge kusimama kwa
dakika moja kuwakumbuka wanafunzi hao, walimu na dereva wao.
Akielezea
utaratibu huo wa michango, Ndugai alisema wabunge hao walikubaliana kuwa kiasi
hicho cha fedha kitagawiwa sawa kwa wafiwa wote.
Ndugai alisema rambirambi
hizo za wabunge zilitolewa kwa makubaliano ya wabunge wote.
0 comments:
Post a Comment