Mwandishi Wetu
![]() |
Humphrey Polepole |
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amekabidhi vyeti 402 kwa wanachama wa CCM
wanaotarajia kuhitimu elimu ya juu katika vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma.
Polepole alikabidhi vyeti hivyo katika
ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM makao makuu ambako viongozi mbalimbali wa
chama na Serikali walihudhuria.
Akizungumza na wahitimu hao, Polepole
aliwataka kuwa mfano mwema katika jamii kwani
hiyo ndio sifa ya mwana CCM.
Aidha aliwasisitiza wale wenye sifa na
vigezo wasisite kuomba nafasi ndani ya CCM katika wakati huu ambao CCM ipo
kwenye uchaguzi wa ngazi zote na jumuiya zote.
“Nawahakikishia CCM mpya hakuna mtu
atakayehujumiwa akiomba uongozi kinachotakiwa ni kuzingatia maadali,” alisema.
Alisema CCM inajali makundi yote, hivyo
kila mwanachama ana haki ya kugombea bila kuhofia mwingine ila kinachotakiwa ni
kufuata taratibu ili kutochafua chama.
Kwa upande wake, Katibu wa Idara ya Vyuo
Vikuu, Daniel Zenda alisema wao wamejipanga kujenga vijana wa vyuo mbalimbali
kukiamini na kujenga chama jambo ambao limeanza kutumia.
Zenda alisema vijana katika vyuo vingi
nchini wameonesha kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo akaiomba
CCM kuwapa ushirikiano ili kukidhi malengo yao.
Alisema katika vyuo wapo wanafunzi wengi
ambao ni wana CCM ila hawapendi kujionesha moja kwa moja ili kuepusha
migongano.
0 comments:
Post a Comment