VATICAN CITY, Vatican
Donald Trump na Papa Franci |
BENDERA pekee ya Marekani ilionekana jana
ikipepea kwenye lango la kuingilia kwenye kasri la Papa Francis lililoko jijini
hapa, wakati Rais wa Taifa hilo kubwa, Donald Trump alipowasili ikiwa ni siku
yake ya tatu kutembelea vyanzo vya dini kubwa duniani.
Trump alikutana na Papa Francis katika
siku yake ya tano ya ziara yake ya kwanza ya urais, baada ya kutembelea vyanzo
vya dini za Uislamu na Uyahudi.
Wakati mazungumzo yao yakibaki siri,
Rais huyo alikuwa na ujumbe mfupi kwa ajili ya Francis wakati akiondoka:
“Sitasahau ulichokisema.
“Ni heshima kubwa,” alisema wakati
akishika mkono wa Papa nao kupiga picha ya pamoja kwenye ghorofa ya pili ya
Sala del Tronetto, ambacho ni chumba kidogo cha Utawala.
“Ahsante sana. Hii ni heshima kubwa
sana,” Trump alisikika baadaye akisema wakati Francis amekaa upande wa pili wa
dawati wakitazamana tayari kuanza mazungumzo yao, kwenye chumba chake cha
faragha cha kujisomea.
Francis ambaye ni mtu asiyependa
kufichaficha mambo, lakini wakati wote huo alikaa kimya.
Baada ya kutoka kwenye mazungumzo yao,
Francis alionekana muda wote akitabasamu kila alipokutana na wana familia hiyo
namba moja ya Marekani.
“Unampa chakula gani?” Francis alimhoji
Melania Trump kwa Kiitaliano, akimaanisha jinsi Rais alivyo na umbo kubwa.
“Pizza nyingi?” “Pizza!?” Melania
aliuliza kwa mshangao huku akicheka.
Papa alibusu Rosari aliyokuwa nayo
Melania mkononi, kabla ya kumsalimia Ivanka Trump na mumewe, Jared Kushner,
sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson na maofisa wengine wa
Marekani.
Baada ya mkutano na Papa, Melania
alizuru hospitali ya watoto inayomilikiwa na Vatican. Alimwambia Francis:
“Nimefarijika sana kutembelea hospitali hii ya watoto wachanga”.
Ziara ya Ivanka ilijumuisha pia kukutana
na waathirika wa biashara ya binadamu na kuandaa mijadala mbalimbali na
wanachama wa Jumuiya ya Sant’Egidio, kikundi cha kijamii cha kutetea haki cha
Kanisa Katoliki.
Familia ya Trump ilikuja na zawadi mbili
kwa ajili ya Papa, ikiwa ni pamoja na kasha la toleo la kwanza la vitabu vya
Mchungaji Martin Luther King, Jr. “Nadhani utavifurahia,” alisema Trump.
Rais pia alimpa sanamu ya shaba nyeusi
yenye maandishi ya ‘Panda Juu’, ikiwa na umbo la yungiyungi lililochanua.
Francis naye alijibu kwa kumpa medali
kubwa iliyosanifiwa na msanii wa Kiroma – taswira ya mti wa mzeituni, kama
alama ya amani.
“Tunaweza kutumia amani,” Trump alijibu.
“Nimeisaini maalumu kwa ajili yako,” Francis alimwambia. “Ooh,” Trump alijibu.
“Hiyo nzuri sana.”
Rais pia aliahidi kusoma nakala tatu za
Waraka wa Baba Mtakatifu alizopewa na Francis – mojawapo ni ‘Lautado si’ yake, ambayo
ni tasnifu inayozungumzia hifadhi ya mazingira. Zingine mbili zinahusu familia
na Injili.
0 comments:
Post a Comment