Grace Gurisha
Thomas Ngawaiya |
TAASISI ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (Cegodeta),
imesema imepata malalamiko mengi ya watu kuhusu fedha za maafa na rambirambi
kwenda kufanya shughuli nyingine, wakati tayari Serikali ilishatenga bajeti ya
kazi hizo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya alisema malalamiko hayo mengi yalikuwa ni yale ya
watu waliyopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera na rambirambi za
wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vincent iliyopo Arusha, waliyopata ajali ya gari.
Ngawaiya alisema watu wanalalamika fedha zao kwenda
kutengeneza barabara, bila kujali kuna watu wameumia na wanahitaji msaada wa
kuwavusha pale walipo kutokana na matatizo waliyoyapata.
Alisema Serikali inatakiwa iliangalie suala hili kwa jiko
la pili la huruma kwa sababu watu wamekata tamaa, kutokana na kwamba wanajitoa
kwa moyo wote kuchangia fedha kwa watu waliyopata matatizo halafu zinakwenda
kufanya mambo mengine jambo ambalo si jema.
“Watu wamekata tamaa kwa sababu wanajitolea fedha nyingi
ili ziende kwa walengwa, lakini hazifiki na mwisho wa siku wafiwa ndiyo
wanaingia gharama, wakati Serikali ilikuwa na bajeti yake,”alisema Ngawaiya.
Alibainisha kuwa kama mambo haya yataendelea hivi watu
watashindwa kujitoa, kwa sababu wao wanatalaji msaada uende kwa walengwa,
lakini hazifiki ambapo kiutawala bora si sahihi kufanya jambo kama hilo.
Alisema kinachotakiwa kufanywa na Serikali ni kuwahesabu
watu waliyopatwa na matatizo hayo na kugawa michango, ndiyo maana watu
walichanga ili zigawanywe na si kuzikupatia na kufanyia shughuli zingine.
0 comments:
Post a Comment