Mwandishi Wetu
Rais John Magufuli |
RAIS John Magufuli amewahakikishia ushirikiano
wafanyabiashara na wawekezaji wa Shirikisho la Taifa la Utengenezaji Mitambo ya
Viwanda la China (CNMIF).
Amesema Serikali yake itawapa
ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa
nishati ya umeme, viwanda na kilimo nchini.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana
Ikulu, Dar es Salaam alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF ambaye ni Mbunge
wa Bunge la Wananchi wa China, Zhan Xin.
Alisema Tanzania imejiwekea malengo ya
kuongeza uzalishaji umeme kutoka megawati 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi
sasa hadi 10,000.
Rais alisema ili kufikia malengo hayo,
wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama
vile gesi, makaa ya mawe na jua.
“Xin kawaambie wawekezaji wenzako wa
China waje Tanzania, nchi zetu ni ndugu na marafiki wa miaka mingi, ili kuunga
mkono juhudi zetu za kujenga viwanda kwa kuzalisha umeme mwingi na pia
kushiriki miradi mingine ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara,”
alisema.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana
na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak na kuzungumzia utekelezaji wa mambo ya ushirikiano na miradi ya maendeleo
iliyotokana na makubaliano ya mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa,
uliofanyika hivi karibuni.
Pia Rais Magufuli alikutana na Kaimu
Balozi wa Uturuki nchini, Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea
Kusini, Songwon Shin.
0 comments:
Post a Comment