Suleiman Msuya
Isaya Mwita |
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya
Mwita, ameahidi kusaidia kupunguza deni la Sh milioni 16 linalodaiwa na
Mkandarasi wa Kampuni ya Ushirombo kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa makaburi ya
Tambaza.
Alisema hayo jana wakati wa dua maalumu
ya kumwombea marehemu Shekhe Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha Mwezi Mtukufu
wa Ramadhan.
Mwita alisema kwa nafasi yake
atajitahidi kusaidia kupunguza deni hilo kama si kulimaliza kabisa kutokana na
umuhimu wa watu waliopumzishwa katika eneo hilo.
Alisema hafanyi jambo hilo kisiasa ama
kufurahisha Waislamu, bali ni kutokana na kutambua umuhimu wa watu waliolala
eneo hilo.
“Nimesikia kwenye risala yenu, kuwa mna deni
la ujenzi wa uzio wa makaburi, sitasema nitachangia kiasi gani, ila nitapunguza
kwa nafasi yangu kiasi ambacho mnadaiwa,” alisema.
“Watu ambao leo hii tunawakumbuka
wamelala hapa, walikuwa na mchango mkubwa, kila mmoja anatambua hilo,
waliitangaza nchi yetu kwenye mambo ya dini na ya kimaendeleo,” aliongeza.
Aidha, Mwita aliwasihi waumini wa dini
ya kiisilamu, katika kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, wajikite katika kuendeleza
mambo mema.
Alisema ufike wakati kila muumini, kutambua
umuhimu wa kutenda na kuendeleza mema aliyofanya wakati wa Mfungo, kwani kufanya
hivyo kutamweka kwenye nafasi nzuri kiimani.
0 comments:
Post a Comment