Grace Gurisha
Askofu Gwajima |
MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, George Milulu,
ameieleza mahakama kuwa alisikia uvumi kwamba Askofu Mkuu wa kanisa hilo,
Josephat Gwajima (47) amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es
Salaam.
Milulu aliyaeleza hayo juzi mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akiongozwa na wakili wake, Peter Kibatala kutoa
utetezi wake katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi inayomkabili
Askofu Gwajima.
Alidai kuwa Machi 29, 2015 alikuwa hospitali ya TMJ,
ambapo alikwenda baada ya kupata taarifa ya uvumi kwamba Askofu Gwajima
amekufa.
Alieleza kuwa alipofika hospitalini alikuta watu ni
wengi, lakini muda mfupi baadaye waliamuliwa na polisi wakae eneo moja ikiwamo
waliokuwa waumini waliokuwa juu ya ghorofa ambapo waliamriwa washuke chini.
Mchungaji huyo alidai licha ya kutoambiwa sababu ya
kutakiwa wakusanyike eneno moja, ilitolewa amri nyingine ya kuwqataka waingie
ndani ya gari la polisi aina ya Land cruiser na kupelekwa kituo cha polisi
Oysterbay.
Alieleza kuwa walipofika kituoni hapo waliamriwa wavue
mikanda, viatu na kuingizwa rumande ambapo wakaanza kutolewa mmoja mmoja na
kuhojiwa. Hata hivyo, alikataa kuliona begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali
vya Gwajima ikiwamo bastola.
Naye, shahidi George Mzava alieleza kuwa hajawahi kukutwa
na begi lolote katika hospitali ya TMJ kama ilivyoelezwa kwenye hati ya
mashtaka. Alidai baada ya kukamatwa na polisi walifikishwa Kituo cha Polisi cha
Oysterbay ambapo waliamriwa wavue mikanda na kuanza kuhojiwa mmoja mmoja.
Alipoulizwa na Kibatala kwamba anazijua sababu za
kuingizwa mahabusu, alieleza kuwa hawakuambia sababu na walikuwa wakiandika
maelezo kwa shinikizo.
Katika kesi hiyo, mbali ya Askofu Gwajima washtakiwa wengine
ni George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wao
wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta
pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.
Wanadaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ
iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki bastola aina ya berretta yenye namba
ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha
na milipuko.
0 comments:
Post a Comment