Mary Mtuka
VIJANA wametakiwa kuwa makini katika biashara wanazofanya kwa kuziweka katika hali nzuri ili kuwavutia wawekezaji.
Aidha kutumia ubunifu na mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye monesho ya Ubunifu ya Sahara Sparks ambayo yamewakutanisha vijana zaidi ya 1200, Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Hassan Mshinde alisema Tanzania bado ipo nyuma katika sekta ya ubunifu ikilinganishwa na nchi nyingine kama za Kenya na Uganda.
Alisema Tanzania inaendelea kubaki nyuma kutokana na kampuni za biashara hasa za vijana kufanya vibaya katika ushindani wa biashara za soko la kimataifa.
"Naamini kuwa maonesho haya yatasaidia kuamsha hamasa kwa vijana wa Kitanzania katika kujikita kwenye ubunifu wa biashara na kampuni zitakazoleta ushindani na hatimaye itasaidi kupunguza changamoto ya ajili kwa vijana," alisema.
Hata hivyo alisema mkutano huo ni fursa kwao kuweza kupanua mawazo yao kupitia wabunifu wa kampuni na wafanyabishara waliofanikiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Venture, Jumanne Mtambalike ambao ndiyo waandaaji wa maonesho hayo alisema lengo la kuanda maonesho hayo ni kuakikisha wana waanda na kuwasaidia vijana mawazo waliyo kuwa nayo ili muwekezaji kuweza kukubali kuwekeza.
Alisema maranyiki kila kija anakuwa na ndoto za kufikia mbali hivyo kuwa kutanisha kwa pamoja na kusikiliza mawazo yao inaweza kuchangia kupata wafanyabiashara wenye ndoto za kufika mbali.
"Kutokana na hilo kampuni yetu imeamuwa kuwafikia vijana hawa katika sehemu mbalimbali za Vyuo zaidi ya 12 kuwaambia waandae mawazo waliyo kuwa nayo ya ujasilia mali ili kufanya biashara zao kuwa za kimataifa," alisema.
Mtambalike alisema mbali na kampuni hiyo wapo wadau mbalimbali ambao wamejipanga kuwasaidia vijana katika kupitia ubunifu teknoloji na ujasilia mali hivyo ni fursa ya kipeke kwa vijana wa Tanzania.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment