Kizimbani kwa wizi kwa udanganyifu


Jemah Makamba

MKAZI wa Kitunda, Ally Salehe (30) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu mali ya Casta Emmanuel.

Akisoma mashtaka hayo jana mbnele ya Hakimu John Msafiri, mwendesha mashtaka Munde Kalambola, alidai kuwa mshitakiwa huyo alifanya tukio hilo akiwa kwenye benki ya CRDB, tawi la Water Front.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa akiwa na mlalamikaji alimwambia ampe Sh milioni 9 ili amwagizie gari aina ya Noah na kumpa.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mshitakiwa alikana kosa hilo na mwendesha mashitaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.

Hakimu alisema kutokana na mshitakiwa huyo kuwa mahabusu kwa makosa mengine mawili yanayomkabili, hawezi kusomewa masharti ya dhamana.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 6 na mshitakiwa alirudishwa rumande.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo