Mwandishi Wetu
WAUGUZI katika Mkoa
wa Pwani wamelalamikia kukosa sare za kazi, hivyo kulazimika kujinunulia
wenyewe, baada ya mamlaka kushindwa kuwapa fedha za kununua.
Hayo yalielezwa
na mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi mkoani humo, Elias Bulole alipokuwa
akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema licha ya
mafanikio wanayopata kazini, ikiwamo kuinua huduma za afya, kutopewa fedha
kwa ajili ya kununua za sare za kazi ni moja ya changamoto zinazowakabili.
“Pia
tunakabiliwa na upungufu wa dawa na vitendea kazi bora katika vituo vya kutolea
huduma,” alisema Bulole.
Mwenyekiti huyo
pia alitaja ukosefu wa nyumba za karibu na maeneo ya kazi, wauguzi wanaojiunga
na masomo ya kujiendeleza kutolipiwa ada na kuchelewa kupandishwa vyeo kuwa ni
changamoto zingine zinazowakabili.
Pia alitaja kutokuwepo
kwa maji katika vituo vya afya na zahanati kuwa ni kero inayowafanya wauguzi
kufanya kazi katika mazingira magumu.
Alisema katika
idara ya afya mkoani Pwani asilimia 80 ya kazi za afya zinafanywa na
wauguzi na kwamba kwa sababu hiyo ni vyema wakapewa kipaumbele katika mambo
mbalimbali.
“Tupewa elimu ya
kutosha, mazingira mazuri ya kazi sanjari na uongezaji wa wauguzi kutoka ni 891
tuliopo sasa hadi 2,591wanaohitajika,” alisema Bulole.
Mkuu wa Wilaya
ya Kisarawe, Happiness Seneda alikiri kuwepo changamoto hizo na kuahidi kuwa
serikali ya wilaya itajitahidi kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
Seneda alisema
wauguzi wote wanafanya kazi ya Mungu hivyoo ni vyema wakaendeleza tabia ya
unyenyekevu kwa wagonjwa.
Katibu wa Afya
mkoa wa Pwani Alfred Karaba alisema changamoto za wauguzi zinajulikana lakini
mafungu yanayotoka serikalini bado hayatoshelezi ambapo alishauri kila halmashauri
kuzitatua kulingana na mafungu wanayopewa.
0 comments:
Post a Comment