Mashaka Mgeta
Mashaka Mgeta |
NI dhahiri kwamba uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) kwa upande wa upinzani katika Tanzania, ulizongwa na hisia za
‘mizengwe’, matakwa ya siasa za ndani ya nchi na kukomoana.
Lakini wapo
walioamini kwamba upinzani, hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), hakikutumia uwiano wa jinsia kuwasilisha majina ya wagombea wake
katika hatua ya awali iliyowahusisha Ezekiel Wenje na Lawrence Masha.
Wawili hao waliteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa EALA,
lakini kura zao hazikutosha, hivyo Bunge (ingawa kwa kushutumiwa kutumika kwa
maslahi ya kisiasa) lilikiamuru chama hicho kuwasilisha majina ya wagombea kwa
awamu ya pili.
Chadema ikawasilisha majina ya Profesa Abdallah Safari,
Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na Pamela
Massay. Miongoni mwao, Lamoyan na Maassay walishinda.
Zipo hekaya nyingi zinazoenea kuhusu kukataliwa kwa Wenje
na Masha, nyingine zikielekezwa katika hofu kwamba kupitia ubunge huo, wawili
hao wangeimarisha nguvu za upinzani katika ukanda wa Ziwa Victoria. Inasemwa
hivyo.
Wapo wanaoamini wana uzoefu katika masuala ya kikanda na
kimataifa, Wenje alikuwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa wakati Masha alifikia hatua ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Kwa nyadhifa hizo, wawili hao walitarajiwa kutoa mchango
mkubwa katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi kupitia EALA, lakini walikataliwa
kwa awamu mbili na wabunge. Lakini iwe iwavyo, Wenje na Masha hawataingia EALA
wakitokea upinzani hususani Chadema, bali Lamoyan na Maassay watakaoungana na
Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahaya, Dk Abdallah Makame, Dk
Ngwaru Maghembe na Alhaj Adam Kimbisa (wote kupitia CCM) na Habibu Mnyaa (CUF).
Pamoja na hali ilivyokuwa katika kuwapata wabunge hao,
sasa nchi inapaswa kuwa katika ‘umoja timilifu’ inapojielekeza katika maslahi
yake kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Tanzania haipaswi kuziibua tofauti
za siasa za ndani zijikite katika EALA. Itakuwa ni kujiangamiza.
Ikumbukwe kwamba EAC ni jumuiya yenye nchi sita zilizo
wanachama, zikiwamo waasisi wake Tanzaia, Kenya na Uganda zilizosaini
makubaliano ya kuanzishwa kwake Novemba 3, 1999 na utekelezaji wake kuanza
rasmi Julai, 7, 2000.
Nchi nyingine ni Rwanda na Burundi zilizosaini mkataba
huo Juni 18, 2007 na kuwa wanachama kamili kuanzia Julai, Mosi, 2007. Sudan
Kusini iliyo mwanachama mpya ilisaini mkataba huo Aprili, 15 mwaka jana na kuwa
mwanachama kamili Agosti, 15 mwaka jana.
Ni jumuiya yenye watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni
150, miongoni mwao asilimia 22 pekee wakiwa wanaishi maeneo ya mijini, hivyo
kuifanya asilimia kubwa (asilimia 78) kuishi vijijini, wengi wao wakijishughulisha
na kilimo na ufugaji. Hivyo kuwa katika EALA si suala la ‘lelemama’, si fursa
ya kuendeleza u-CCM, u- Chadema ama u-CUF.
EALA ni jukwaa lenye kusimamia kwa dhati maslahi ya nchi
ndani ya mkataba uliosainiwa na kuzishirikisha nchi sita. Itakuwa fedheha na
Tanzania itachekwa na dunia ikiwa wabunge waliochaguliwa kuingia EALA watajikita
katika tofauti zinazotokana na siasa za ndani, wakiwaacha wabunge wenzao
wakizitetea nchi zao na maslahi yanayogusa maisha ya watu wao. Ijulikane kwamba
pamoja na kuwa na Jumuiya ya kikanda, kila nchi inabaki kuwa na maslahi yake
binafsi yanayoweza kuathirika kupitia uamuzi unaochukuliwa baada ya mijadala
inayofanyika ndani ya EALA.
Kwa maana EAC ni ukanda unaochochea ushirikiano na
muingiliano katika maeneo tofauti kwa maslahi ya kila upande. Maeneo hayo ni
pamoja na siasa, uchumi na jamii.
Kwa sasa, ushirikiano wa kikanda unaendelea vema katika
masuala ya ushuru wa forodha, uanzishwaji wa soko la pamoja na utekelezaji wa
itifaki ya sarafu moja katika ukanda huo.
Lakini yapo masuala mengi kuanzia KWA Ujinga Wangu
nimejaribu kuangalia utendaji wa baadhi ya viongozi wa zama hizi na zilizopita na
kubaini kuna tofauti kubwa ya utendaji wa kazi.
Ninasema hivyo kwa sababu kwa umri nilionao nimeona awamu
nyingi za uongozi ndani ya nchi yetu na namna walivyofanya shughuli zao. Zama
zile waliamini kwenye kutumikia wananchi kutoka moyoni na walifanikiwa kwa
kiwango kikubwa.
Tena wakati huo wala hakukua na vyombo vingi vya habari
kama ilivyo sasa. Walikuwa na njia ambazo walitumia kuwasaliana na wananchi wao
katika masuala mbalimbali ya maendeleo. Ilikuwa ni nadra kuwaona wakikimbilia
kwenye vyombo vya habari kujieleza walichofanya.
Utendaji wao ulijionesha wazi kwa wananchi kwa namna
walivyosimamia majukumu yao. Sikuona iwe mkuu wa mkoa wa mkuu ama wilaya wakitumia
vyombo vya habari mara kwa mara ili kuonesha waliyoyafanya.
Kwa Ujinga Wangu hii ni kwa sababu waliamini utendaji
kazi unaweza kujulikana kwa wananchi bila hata kutumia chombo cha habari.
Viongozi waliopita waliamini utendaji kazi wao unaonekana moja kwa moja kwa
wananchi na si kutumia vyombo hivyo kujitafutia umaarufu.
Nimeamua kujadili mada hii baada ya kuona baadhi ya
viongozi wanatumia muda mwingi na nguvu kubwa kutafuta fursa ya kuzungumza
kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia nafasi waliyonayo kushughulikia
matatizo ya watu.
Kwa Ujinga Wangu kwa kusema hivyo sina maana kuwa wakuu
wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine serikalini wasitumie vyombo vya
habari, hapana bali wavitumie kwenye mambo ya msingi ambayo umma lazima
ujulishwe.
Nafahamu chombo cha habari kinarahisisha kufikisha ujumbe
wa kiongozi kwa wananchi wake kwa haraka zaidi na hivyo lazima vitumike lakini
si kwa kila jambo.
Siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya wakuu
wa mikoa kuona chombo cha habari ndiyo kimbilio lake.
Asipoonekana kwenye runinga anahisi anaumwa na yupo
tayari ku-ACHA NIPAYUKE Mashaka Mgeta ngazi za kitaifa hadi zile za msingi
zinazowagusa wananchi wa kawaida walio walengwa wakuu katika ushirikiano huo.
Uhusiano wa raia wa mataifa hayo upo katika maeneo yenye
tija na faraja, lakini pia katika mizozo inayoweza kuhatarisha usalama, mali na
maisha ya watu.
Hayo ni baadhi ya mambo machache kati ya mengi ambayo
wabunge wa EALA kutoka Tanzania wanapaswa kuyatilia mkazo, kuyajua kwa kina na
kuyahusisha na misimamo katika sera za nje za nchi, ili kila watakapotimiza
wajibu wao, waiweke Tanzania na Watanzania mbele ya vyama vyao.
Itakuwa ni kuukwepa ukweli kwamba hisia za kuwa
‘mizengwe’ katika uchaguzi wa mwaka huu hususani katika kambi ya upinzani,
hazipaswi kupuuzwa. Madhara yanayoweza kutokana na matokeo ya ‘mizengwe’ hiyo
hayataviathiri vyama vya siasa bali Tanzania na Watanzania.
Lakini kama walivyosema wahenga, maji ukiyavulia nguo,
hauna budi kuyakoga. Sasa wabunge waliobainika kuwa wenye maslahi kwa nchi
kupitia kwa wawakilishi wa wananchi, wameshachaguliwa kuingia katika EALA.
Jambo la msingi ni kutoziendekeza siasa za ndani na
tofauti. Kama uchaguzi huo, pamoja na ‘mizengwe’ inayotajwa ulikuwa wenye heri
basi heri hiyo iendelee kuwapo, lakini ikiwa itaibua shari, basi Watanzania
waungane kuliepusha Taifa na shari zote, ushindi utakuwa kwa wote.
0 comments:
Post a Comment