Dk Mohamed Shein |
WANANCHI wa Zanzibar, wamehimizwa
kuchangamkia fursa zilizopo katika Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) na kuondokana na dhana kuwa Serikali yao inabaguliwa.
Akiwasilisha mada kuhusu ushiriki wa
Zanzibar katika EAC kwenye semina ya masuala ya mtangamano, Ofisa wa
Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Suleiman Haji alitoa ufafanuzi wa kina kuonesha namna Zanzibar
inavyoshiriki kwenye EAC.
Haji alieleza kuwa licha ya Zanzibar
kuwa sehemu ya Muungano Tanzania, ushiriki wake umedhihirika katika mgawanyo wa
miradi ya maendeleo ya EAC, hususan miradi ya miundombinu.
Alisema Zanzibar iliwasilisha
mapendekezo ya miradi 10 kwenye Sekretarieti ya EAC na kutokana na vipaumbele
vilivyowekwa miradi mitatu imekubaliwa na mchakato wa kuitekeleza unaendelea.
“Mradi wa Bandari ya Marhubi Kisiwani
Pemba, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ununuzi wa meli kubwa
zitakazosafirisha abiria na mizigo kwenye nchi wanachama wa EAC.
Aidha, alisema Zanzibar inanufaika na
miradi inayofadhiliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya kukuza biashara
na kupunguza umasikini katika nchi za EAC inayoitwa "East Africa
Trademark" (TMEA).
Alisema mradi mwingine unaofadhiliwa na
TMEA huko Zanzibar ni ule wa kuwasilisha malamiko kwa njia ya mtandao au ujumbe
mfupi wa simu pale inapotokea mfanyabiashara amekumbana na vikwazo visivyo vya
forodha katika kusafirisha bidhaa zake ndani ya Jumuiya.
Ofisa huyo alisema Benki ya Dunia (WB), inaendesha
mradi wa kutathmini utekelezaji wa Soko la Pamoja kwa upande wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment