Suleiman Msuya
Zitto Kabwe |
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe,
amesema Tanzania inapaswa kuhakikisha sheria na sera za madini zinalazimisha rasilimali
madini kuwa mali ya Watanzania ndipo nchini itanufaika.
Aidha, amesema ni wakati muafaka kwa Taifa
kujitoa katika mfumo wa kodi za Kimataifa akiuelezea kuwa umeonesha kunyonya
nchi maskini zaidi na kunufaisha zile tajiri.
Zitto alisema hayo jana wakati
akizungumza kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na televisheni ya
Azam Dar es Salaam.
Alisema kwa kuwa Rais John Magufuli
ameamua kupigania vita hiyo ni jukumu la kila Mtanzania kupigana hadi
kuhakikisha kuwa madini yanakuwa ni mali ya wananchi wa Kitanzania.
Zitto alisema kwa mujibu wa sheria
iliyopo inaanisha kuwa baada ya mwekezaji kuingia mkataba na Serikali madini ni
mali yake jambo ambalo halikubaliki.
“Hii vita ni vita ngumu ila kwa sababu
Rais ameamua kuipigana pamoja na ukweli kuwa anajua jitihada za Serikali
iliyopita tunapaswa kumuunga mkono ili tuweze kunufaika.
“Mimi nataka mambo haya mawili yaangaliwe
ili kuhakikisha kuwa rasilimali madini inatambulika kama mali yetu kwani kwa
sasa ni mali ya mwekezaji,” alisema.
Alisema iwapo sheria inapaswa kumtambua
mwekezaji kama mkandarasi kwani kwa sasa inamfanya aonekane ndiye mwenye mali.
Mbunge huyo alisema kwa mujibu ya sheria
ya gesi na mafuta mwekezaji ni mkandarasi ambapo akipata bidhaa husika
anarejesha gharama yane na katika faida nchi inagawana na mwekezaji kwa sawa au
nchi kupata zaidi.
Alisema jambo la pili ni mfumo wa kodi
wa kidunia umeweka mazingira ambayo kampuni za Kimataifa zinauwezo wa kuhamisha
mapato yake kwenda kwenye visiwa ambavyo kodi zipo chini hali ambayo inachangia
wasilipe kodi.
Mbunge huyo alisema mfano mwaka 2011
Kampuni ya Barick wakati huo ambayo kwa sasa ni Acacia ilitoa taarifa ya kupata
hasara nchini ila ilionesha kupata faida nchini Uingereza hivyo kulipa kodi kwa
Malkia.
Zitto alisema katika kukabiliana na hali
hiyo dunia ilianza mjadala wa kuhakikisha kuwa kodi hizo zinapatikana na
Tanzania ilikuwa ni mwenyekiti wa mjadala huo ila tangu Serikali ya awamu ya
tano iingie madarakani imeonekana kuachwa.
“Ni masikitiko makubwa kwa Serikali ya
Tanzania kuacha mjadala ambao tulikuwa tunaongoza wa mfumo wa kodi za Kimataifa
ambao ungeweza kutuletea mabadiliko chanya ya rasilimali madini ambayo
inaonekana haina faida kwa nchi na wananchi,” alisema.
Mbunge huyo alisema tipoti ya Profesa
Abdulkarim Mruma haina jipya katika ripoti ya Jaji mstafufu Mark Boman ambayo
ilianisha yote yaliyoanishwa kwa sasa.
Zitto alisema kamati hiyo ilipendekeza
miaka tisa iliyopita kuwepon kwa mashine ya uchenjuaji inakuwepo ikiwa ni
pamoja na kuwepo sera na sheria sahihi kwa sekta hiyo.
“Nakumbuka nilikuwa masomoni nchini
Ujerumani nilirudi kupitisha sheria hiyo ambayo ilipangiwa kutumia wiki moja ila
muda haukutosha ikawa wiki mbili na tulishirikisha watu asasi za kiraia ili
kutusaidia kupata mkuafaka,” alisema.
Mbunge huyo alisema kwa ushirikiano huo
ilikuwa rahisi wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kufanya kazi na
kuja na mapendekezo sahihi kuhusu rasilimali hiyo.
Alisema wao kama chama wamejipanga
kufanya mjadala mwisho wa wiki hii kuhakikisha jamii inatambua rasilimali
madini kwa undani ili kila mtu aweze kufahamu kila kitu.
Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana alisema ni wakati muafaka
wa Watanzania kujitathmini kuwa wana matatizo gani.
Alisema ni vema kuangalia uwezekano wa
kutumia wataalam mbalimbali duniani kuhusu rasilimali zake ili ziweze
kunufaisha jamii kwa ujumla.
Bana alisema ukifuatilia mfumo wa
kutunga sera na sheria za nchi unaonekana kufuata misingi nataratibu
zinazohitajika ila kumekuwepo na changamoto ya usimamizi na utekelezaji.
“Wakati mwingine najiuliza tunakwama
wapi ila nabakia na tafsiri mbili kwamba kuna mashinikizo ya wazi na yasiyo ya
wazi hivyo tunapaswa kujipanga kukabiliana na hali hiyo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment