Mwandishi Wetu
Jaji Semistocles Kaijage |
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi ya
ubunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema kuwa wazi.
Uamuzi huo umekuja baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa
Viti Maalumu wa chama hicho, Dk Elly Macha, aliyefariki dunia Machi 31.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles
Kaijage, alitangaza nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya
Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343.
“Tayari Spika wa Bunge ameijulisha Tume juu ya kuwepo kwa
nafasi wazi ya mbunge huyo,” alisema Jaji Kaijage.
Alisema taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa
kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya
Uchaguzi, Sura ya 343.
Dk Macha alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu bungeni
hadi alipofariki dunia akiwa Uingereza kwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment