Ndumey Mukama (katikati) |
CHAMA cha Wapangaji nchini kimesema kwa
sasa kiko kwenye mchakato wa kuandaa sera ya ardhi ambayo itambana mpangaji na
mpangishaji ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo hususan upandishaji
kodi.
Akizungumza na JAMBO LEO jana, Katibu
Mkuu wa Chama hicho, Ndumey Mukama, alisema kwa kiasi kikubwa kukosekana sera
hizo kumekuwa kukisababisha watu hao kukosa pa kujitetea.
Alisema baada ya mchakato wa kutoa maoni
unaoendelea sasa, kukamilika sera hiyo itapelekwa kwenye Baraza la Mawaziri ili
ijadiliwe na kisha kupelekwa bungeni, ambako kwa mara ya kwanza itasomwa kwenye
Bunge lijalo.
"Tutakuja na sera ambayo
itamwezesha mpangaji au mpangishaji kupanga gharama anayoitaka kwa kuwa kwa
sasa haipo hivyo tunashindwa kuwabana kwa mujibu wa kanuni na sheria ambapo
kila mmoja ataifuata," alisema.
Aliongeza kuwa kwa kiasi kikubwa
wamekuwa wakikemea hatua ya wenye nyumba kupandisha kodi, lakini kutokana na
kuwa hakuna sera ya nyumba wanafanya wanavyotaka jambo ambalo huleta kero kwa
wahusika.
0 comments:
Post a Comment