Mwandishi Wetu
Rais John Magufuli |
MBUNGE wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF),
ametaja baadhi ya mambo katika 34 yaliyomfanya kupiga kura ya ‘ndiyo’ kwenye
mchakato wa upitishaji Bajeti kwa mwaka 2017/18.
Baadhi mambo hayo ni pamoja na Bajeti
kutetea rasilimali za madini, kuondoa kodi kwenye maeneo mengi yanayogusa
wananchi na kuondoa tozo zilizokuwa zikitesa wafanyabiashara.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Nachuma
alisema kwa kiasi kikubwa kuoendolewa tozo kwenye mazao kutawezesha upatikanaji
chakula kwa wingi na bei haitapanda.
“Mimi mbunge ninayejitambua, nampongeza
Rais John Magufuli kwa kusimamia rasilimali za nchi vizuri licha ya kuwapo watu
wasio na sera wanaoponda anavyofanya, hivyo namsihi akaze buti,” alisema.
Aliongeza kuwa anaunga mkono bajeti zote
zilizopitishwa pamoja na mikataba ya madini iliyosainiwa na kupitishwa na Serikali
ya sasa.
Aidha, alisema mambo mengine katika hayo
34 anatarajia kuyataja katika mikutano yake ya hadhara anayotarajia kuifanya
jimboni hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment