Dk Anna Makakala |
KAMISHNA Jenerali wa Uhamiaji Dk Anna
Makakala amefanya mabadiliko ya viongozi wa Uhamiaji wa mikoa na kuteua wapya
Tanzania Bara na Visiwani.
Mabadiliko hayo yamemgusa Kamishna wa Idara
hiyo Kanda ya Dar es Salaam, John Msumule ambaye ameondolewa na nafasi yake
kuchukuliwa na Naibu Kamishna Mary Palmer.
Kwa mujibu wa taarifa ya Dk Anna,
katika mabadiliko hayo, Sixstus Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza amehamishiwa Simiyu wakati aliyekuwa na nafasi kama hiyo mkoani Rukwa, Selemani Kameya amehamishiwa Tabora.
katika mabadiliko hayo, Sixstus Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza amehamishiwa Simiyu wakati aliyekuwa na nafasi kama hiyo mkoani Rukwa, Selemani Kameya amehamishiwa Tabora.
Aidha, katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Mbeya, Asumsio Achacha amehamishiwa mkoa wa Kaskazini Pemba huku aliyekuwa
Manyara, Peter Kundy akihamishiwa Dodoma kuchukua nafasi ya Ali Mohamed ambaye
amehamishiwa Arusha.
Mkemi Mhina Seif ameteuliwa kuongoza mkoa
wa Kusini Unguja, huku Muhsin Abdallah Muhsin akiteuliwa kuongoza mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Katika mabadiliko hayo pia, Said Omary Hamdani
ataongoza idara hiyo mkoa wa Mjini Magharibi na Othman Khamis Salum anakuwa Mkuu
wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja.
Baadhi ya wakuu wa Uhamiaji wa mikoa
wamebaki kwenye vituo vyao vya kazi vya awali.
Katika mabadiliko hayo, Kamishna
Jenerali Makakala pia aliteua viongozi wapya idara kwenye baadhi ya mikoa
ambapo Plasid Mazengo ameteuliwa kuongoza mkoa wa Pwani huku Mrakibu Mwandamizi
James Mwanjotile akipelekwa kuongoza Mtwara.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope Kawawa
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa na Kamishna Msaidizi wa
Uhamiaji Hosea Kagimbo anahamishiwa mkoa wa Njombe.
Wengine ni Rashid Magetta anakuwa Mkuu
wa Uhamiaji wa Mkoa wa Songwe, Carlos Haule, anakwenda Rukwa; Julieth Sagamiko,
Manyara; Albert Rwelamila, Kilimanjaro na Paul Eranga, Mwanza.
Crispin Ngonyani anakwenda Tanga; Shaban
Hatibu, Katavi; Remigius Pesambili, Kigoma na Novaita Mrosso anakwenda Mbeya.
Aidha, Bakari Mohamed Ameir anakuwa Mkuu
wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
(AAKIA) na Fulgence Mutarasha anakuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
0 comments:
Post a Comment