Jemah Makamba
Salum Njwete ‘Scorpion’ |
SHAHIDI katika kesi inayomkabili
mshitakiwa Salum Njwete ‘Scorpion’, ya kuiba kujeruhi na
kumtoboa macho Saidi Mrisho amedai mshitakiwa huyo ni mlinzi wa amani.
Katika kesi hiyo iliyoendelea
kusikilizwa jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, shahidi
huyo, Deus Magosa alidai anamfahamu hivyo mshitakiwa.
Shahidi huyo mkazi wa Buguruni ambaye ni
kiongozi wa ulinzi shirikishi wa eneo hilo, alidai kuwa yeye ndiye aliyempa
ajira ya ulinzi wa amani mshitakiwa kwenye eneo hilo la biashara ndogondogo.
Mwendesha mashitaka wa Serikali, Nassoro
Katuga alimhoji shahidi huyo namna anavyomfahamu Scorpion ambapo mbele ya
Hakimu Flora Haule, Magosa (46) alijibu anamfahamu kwani mshitakiwa aliajiriwa
na wafanyabiashara wadogo kuwalinda pamoja na biashara zao pamoja na uongozi
wao wa ulinzi ushirikishi.
Aliendelea kudai kuwa Salum alikuwa
akilipwa Sh 10,000 kwa siku na wafanyabiashara hao kwa kuwawezesha kuendelea na
biashara zao bila matukio ya wizi.
Hata hivyo, shahidi huyo alipoulizwa
kama anakumbuka kilichotokea Septemba 6 mwaka jana, Magosa alijibu kwamba siku
hiyo hakuwapo alikuwa msibani nje ya Dar es Salaam
Aliendelea kudai kuwa aliporudi alisikia
watu wakizungumza mtaani, kwamba kuna mtu alitobolewa macho na kujeruhiwa
katika tukio lililotokea maeneo ya Buguruni ambapo walimtaja mshitakiwa kuwa
ndiye aliyehusika na tukio hilo.
Wakili alimwuliza baada ya hapo nini
kiliendelea shahidi akajibu waliitwa Polisi na alipokwenda aliulizwa kama
anamfahamu Salum Njwete ambapo alijibu anamfahamu na kumtaka akamwite.
Shahidi alidai alimfuata mshitakiwa na bila
shaka wala kukataa alisema yeye ni raia mwema na alikwenda polisi bila
kukamatwa na akaambiwa niondoke akamwacha mshitakiwa Polisi Buguruni.
Wakili Katuga alisema kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa Aprili 18 ushahidi utakapoendelea kutolewa.
0 comments:
Post a Comment