Grace Gurisha
RAIA wawili wa India wanaotuhumiwa kuingilia mawasiliano
ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisababishia
Serikali hasara ya Sh bilioni 4.3 wanatarajiwa kupandishwa kizimbani leo kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kusikiliza hatua ya upelelezi
ilipofikia.
Washitakiwa hao ni Kalrav Patel (37) mkazi wa Mazizini,
Zanzibar na Kumal Ashar (59) mkazi wa Mkunazini pia Zanzibar.
Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi,
Cyprian Mkeha, ambapo awali upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo haujakamilika na kuomba siku nyingine ya kukamilisha upelelezi.
Katika mashitaka ya kwanza, washitakiwa hao wanatuhumiwa
kuingiza nchini vifaa vya mawasiliano
bila kibali, katika tarehe zisizofahamika mwaka juzi
wakiwa Zanzibar ambako waliingiza vifaa vya mawasiliano ya sauti katika
intaneti (VoIP) yenye namba 0030F1001903 na Cisco Router namba 12F1070C204574
bila kibali cha TCRA.
Ilidaiwa katika mashitaka ya pili kuwa Patel na Ashar katika
tarehe zisizofahamika Zanzibar, waliweka au walisimika vifaa hivyo vya
mawasiliano bila kibali cha TCRA.
Katika mashitaka ya tatu wanatuhumiwa kutumia vifaa vya
mawasiliano ambavyo havijathibitishwa na TCRA, ambapo walitenda kitendo hicho kati
ya Februari 25 na Aprili 18 mwaka jana Zanzibar.
Hakimu Mkeha aliwaeleza washitakiwa kuwa Mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo kutotakiwa kujibu chochote wala
kupewa masharti ya dhamana, kwani Mahakama Kuu ndiyo inahusika na dhamana yao.
0 comments:
Post a Comment