Suleiman Msuya
James Mbatia |
KATIBU Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda
amesema afya ya Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia inaendelea vizuri na
matarajio yao ni kumwona akishiriki Bunge la Bajeti linaloanza leo, Dodoma.
Aidha, Danda amesema chama hicho
hakirudi nyuma kujijenga na kuwa watu wanaofikiria kuwa kitaharibu malengo yake
hawatafanikiwa.
Katibu huyo alisema hayo jana alipozungumza
na JAMBOLEO na kubainisha kuwa kwa matibabu anayopata Mwenyekiti wao yanamfanya
aendelee vizuri na afya yake inazidi kuimarika.
“Tangu atoke kwenye matibabu amekuwa
akiimarika na kwa sasa hata magongo hatumii kutembea na naamini atashiriki
vikao vya Bunge,” alisema.
Alisema wamejiwekea mikakati ya
kurejesha heshima ya chama, hivyo watu wanaotumika kuharibu mwelekeo wa chama
hawatakubalika.
Katibu Mkuu alisema katika kuonesha
dhamira ya kujenga chama wamemfukuza aliyekuwa mwanachama wao, Faustine Sungura
baada ya kubaini kuwa hana nia njema na chama hicho.
Alisema Sungura amekuwa akishirikiana na
watu kujaribu kuhuju chama, hivyo wasingeweza kumvumilia.
“Sungura amekuwa akitumika na bahati
nzuri hakuwa na cheo hivyo hana madhara lakini katika kurejesha heshima ya
chama Kamati Kuu ilivyokutana hivi karibuni iliamua kumfukuza NCCR-Mageuzi,”
alisema.
Kwa upande mwingine alisema chama hicho
hakina mpango wa kufungua kesi ya kupinga mchakato wa uchaguzi wa wabunge wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kwa kuwa wagombea wa vyama vya CUF na Chadema
ni wana Ukawa wenzao.
0 comments:
Post a Comment