Mery Kitosio, Moshi
Augustine Mrema |
MWENYEKITI wa Bodi ya Parole, Agustino Mrema, amemwomba
Rais John Magufuli amruhusu kutoa wafungwa wenye sifa ya kupata msamaha kutoka
bodi hiyo ili wamsadie kufichua majambazi wanaopora na kuua Polisi.
Pia alisema ana imani majambazi wengi wanaoendesha
matukio ya uhalifu wametokea magerezani au watakuwa na uhusiano na wafungwa.
Mrema alitoa ombi hilo baada ya kumalizika kwa msiba wa
ndugu yake kijijini kwake Kiraracha Marangu mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa ipo kampeni mbaya ya kumchafua Rais Magufuli
katika utawala wake unaofanywa na wahalifu.
"Kwa uzoefu nilionao kuna kampeni chafu ya kumchafua
Rais Magufuli ili nchi isitawalike kwamba hata majambazi wanaweza kuua askari
hivyo kuna kila haja ya kuwashirikisha wafungwa katika tukio hili ili
watisaidie kufichua,"alisema.
Aliongeza kuwa watu wabaya wasioridhika na uongozi wa Rais
Magufuli wanafanya kila mbinu kwa ajili ya kumchafua ikiwemo kufadhili vikundi
vya uhalifu vinavyohatarisha amani ya nchi.
Mrema alisema ili kukomesha matukio hayo ni vema Rais
akaruhusu bodi yake iwakamate na kuwapunguza wafungwa magerezani hasa wale
wenye makosa ya kushindwa kulipa faini ili waweze kufichua wanaohusika na
uhalifu huo.
Pia alimtaka Rais kuthibiti watu wanaoleta chokochoko za
maneno dhidi yake wachukuliwe hatua kwani wameonesha dhahiri hawapendeziwi na
utawala wake kwani ndiyo pia wamekuwa wakifadhili matukio hayo.
Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa kumchagua kuwa
mwenyekiti wa bodi hiyo kwani amejipanga kumsaidia kwa nguvu zote bila kujali
maslahi binafsi na hadi sasa amekuwa hazifanya kazi hizo bila malipo yoyote na
hana mpango wa kumdai isipokuwa atakapoona umuhimu wa kumlipa upo.
0 comments:
Post a Comment