Suleiman Msuya
Profesa Ibrahim Lipumba |
WANACHAMA wawili Masoud Ali Said na
Zainabu Lipalapi walioteuliwa na Profesa Ibrahim Lipumba kushika nafasi
mbalimbali ukiwamo ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF wamekataa uteuzi.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Mkurugenzi
wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma, Mbarala Maharagande.
Alisema hii ni mara ya pili kwa
wanachama wa CUF wanaojitambua kukataa uteuzi wa Lipumba kushika uongozi na
kumweleza wazi kuwa hana mamlaka hayo kwa kuwa alishafukuzwa uanachama.
Maharagande alisema Diwani wa CUF Viti Maalumu
Lindi, Lipalapi alikataa kupokea uteuzi wa kuwa mjumbe wa Bodi ya Wadhamini.
Alibainisha kuwa Lipalapi alisema hatambui
uteuzi huo hivyo amtoe atafute mtu mwingine kuepuka matatizo na familia yake.
Maharagande alisema kutokana na hali
hiyo, Lipumba na wenzake wanampa wakati mgumu Msajili wa Vyama vya Siasa na
vyombo vya Dola, kwa kuwa RITA haiwezi kusajili Bodi yenye wajumbe wanane badala
ya tisa kama Katiba ya CUF inavyotaka.
0 comments:
Post a Comment