Mwandishi Wetu
Edward Lowassa |
WABUNGE 11 kutoka Kenya na wageni mbalimbali jana
walimtembelea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kijijini kwake Ngarash
mkoani Arusha.
Huku wakiongozana na vikundi vya wajasiriamali vya mkoani
humo, wabunge hao walifanya mazungumzo na mbunge huyo wa zamani wa Monduli
ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, alishika nafasi ya pili nyuma ya
Rais John Magufuli.
Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alithibitisha ugeni
wa wabunge hao na kubainisha kuwa walikuwa na ujumbe maalumu kwa Lowassa.
Wabunge hao wanamtemebela Lowassa katika kipindi ambacho
Kenya inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu Agosti.
Licha ya Liongo kutopatikana kufafanua lengo la ziara
hiyo, duru za siasa zinaeleza kuwa wabunge hao walikwenda kuchota uzoefu wa
uchaguzi kwa Waziri Mkuu huyo, ambaye katika uchaguzi wa mwaka juzi alitoa
upinzani mkali kwa chama tawala CCM.
Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8
sawa na asilimia 58.47 akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa
na asilimia 39.97.
Matokeo hayo yalimfanya Rais Magufuli kupata asilimia
chache ya kura kuliko wagombea wengine wa CCM, lakini licha ya uchache huo
amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua tangu
alipoapishwa Novemba 5, 2015.
0 comments:
Post a Comment