Joyce Kasiki, Dodoma
Mama Salma Kikwete |
MBUNGE wa
Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM), ameuliza swali la nyongeza muda mfupi baada ya
kuingia bungeni kwa mara ya kwanza na kuapishwa.
Katika swali
hilo, Mama Salma ambaye ni mke wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alitaka
kujua mpango mahususi wa Serikali kuongeza usambazaji huduma ya Mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), mkoani Lindi.
"Serikali
ina mpango gani wa kuhakikisha inaongeza wigo wa kutoa huduma kwa wananchi
katika mpango wa Tasaf III wa kunusuru kaya masikini hususan kwa mkoa wa
Lindi?” Alihoji.
Akijibu swali
hilo, Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora,
Angelah Kairuki alisema tayari wamesambaza huduma hiyo kwa asilimia 70 mkoani
Lindi.
"Hivi sasa
imebaki asilimia 30 ambayo ni takribani wakazi 350,000 ambayo wanatarajia
kuikamilisha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18.
Awali, katika
swali la msingi, Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohamed Issa (CUF), alitaka kujua
kama Serikali haioni haja ya kuongeza viwango vya ulipaji kwa kaya masikini
hasa ukizingatiwa upandaji wa bei za mahitaji ya kila siku na kuporomoka kwa
thamani ya sarafu yao.
Pia alitaka
kujua ni vigezo gani vya uhakika vitatumika ili kupata kaya masikini ambapo katika
swali la nyongeza, Mbunge huyo alihoji kama Serikali haioni umuhimu
wa kuwapa fedha TASAF kwa mkupuo hata wa miezi sita ili kuongeza tija.
Akijibu maswali
hayo kwa pamoja, Kairuki alisema mpango huo wenye madhumuni ya kuwezesha
kaya masikini kuongeza kipato, fursa na kuinua kiwango cha matumizi yao, ni wa
miaka 10 na unatekelezwa kwa vipindi vya miaka mitano kuanzia mwaka 2013-2023.
Waziri huyo,
alibainisha kuwa vigezo vya kupata kaya masikini huainishwa na jamii katika
mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka halmashauri za wilaya na
kusimamiwa na viongozi wa vijiji, mtaa na shehia.
“Ruzuku
inayotolewa kwa walengwa imeongezwa baada ya kufanyiwa mapitio kwa kuangalia
hali halisi, hata hivyo, ieleweke kwamba viwango vinavyotolewa vilipangwa hivyo
ili kata masikini iendelee kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato
na kutotegemea ruzuku pekee,” alisema Kairuki.
0 comments:
Post a Comment