Celina Mathew
JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini
limekiri kugubikwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa magari.
Jeshi hilo sasa lina magari yasiyozidi
100 wakati mahitaji yake halisi ikiwa ni magari 300, jambo ambalo linafanya
kazi iwe ngumu.
Changamoto nyingine inayolikabili jeshi
hilo ni uhaba wa watumishi, uelewa mdogo wa wananchi kuhusu nini kifanyike
wakati linapotokea janga la moto, miundombinu mibovu ya barabara.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna
Jenereli wa jeshi hilo, Thobias Andengeye alisema licha ya jeshi hilo kupata
mafanikio makubwa, changamoto hizo zimekuwa kikwazo.
Alisema kwa kiasi kikubwa changamoto ya
miundombinu inasababisha magari yanayoenda kuzima moto kunapotokea tatizo
kuchelewa kufika sehemu husika.
Aliwataka wananchi kuwa na tabia ya
kupisha magari hayo pindi yanapokuwa yakipita kwenda eneo fulani kwa lengo la
kudhibiti moto badala ya kuwaambia wanaoendesha kama wana haraka wapiti juu.
Hata hivyo, alisema kwa sasa jeshi hilo lina
ofisi katika mikoa 28 nchini kwenye wilaya tisa na kwamba katika miiko
iliyobaki mchakato unaendelea, huku katika viwanja vya ndege vikiwa 19.
Aidha waliwataka wananchi wanaojenga
nyumba kuhakikisha ramani za eneo zinapimwa ili kuwepo tahadhari ya majengo
pindi moto unapotokea.
Hiyo itasidia kujua moto ukitokea
wawatokea wapi ili kupunguza madhara kwa kuweka milango ya tahadhari na hadi
sasa takwimu za mwaka 2016/2017 zikionesha kuwa maeneo 25,418
yameshakaguliwa,”alisema.
Aliongeza kuwa hadi sasa watu 100,000
wamepewa elimu kuhusu masuala hayo kwa shirikiana na vituo vya redio na
makampuni ya simu kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na Halotel ambapo
wanawajulisha wananchi kupiga namba 114 bure linapotokea tatizo.
0 comments:
Post a Comment