WASHINGTON, DC
Donald Trump |
ANAKUMBUKA udereva, anajihisi kuwa ndani
ya kifukofuko, na anashangaa jinsi kazi yake mpya ilivyo ngumu.
Rais Donald Trump juzi alikumbuka siku
zake 100 za kwanza Ikulu huku akikumbuka maisha yake kabla ya kuingia
madarakani.
“Nilipenda maisha yangu ya nyuma.
Nilikuwa na mambo mengi sana yakiendelea,” Trump aliliambia Shirika la Habari
la Uingereza (Reuters) katika mahojiano maalumu. “Hii ni kazi kubwa kuliko
ilivyokuwa huko nyuma. Nilidhani itakuwa rahisi kuliko.”
Akiwa tajiri kutoka New York, Trump
aliingia madarakani kwa mara ya kwanza alipoingia Ikulu Januari 20 baada ya
kumshinda Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Hillary Clinton.
Zaidi ya miezi mitano baada ya ushindi
wake na siku mbili kabla ya siku 100 za urais wake, uchaguzi bado umo akilini
mwa Trump.
Katikati ya mazuungumzo juu ya Rais wa
China, Xi Jinping, Rais alitulia kidogo ili akabidhi nakala za kile alichosema
ndizo takwimu za sasa kutokana na ramani ya uchaguzi wa mwaka jana.
“Hapa, mnaweza kuchukua hiyo, hiyo ndiyo
ramani ya mwisho ya idadi,” Rais huyo wa Republican alisema akiwa mezani
ofisini mwake, akikabidhi ramani za Marekani na maeneo ambayo alishinda yakiwa
yamewekwa alama nyekundu. “Ni nzuri, sawa? Nyekundu bila shaka ni sisi.”
Alikuwa na nakala kwa kila mwandishi
kati ya watatu hao wa Reuters ofisini mwake.
Trump, ambaye alisema alizoea kutokuwa
na faragha katika “maisha yake ya uzee,” alielezea mshangao wake wa jinsi
anavyobanwa sasa. Na aliweka wazi kwamba anaanza kuzoea ulinzi wa saa 24 pamoja
na udhibiti mwingine unaoendana na hali hiyo.
“Hakika unakuwa umo kwenye kifukofuko
chako mwenyewe, kwa sababu unakuwa na ulinzi mkali vile, kiasi kwamba huwezi
kwenda kokote,” alisema.
Rais anapoondoka Ikulu, kwa kawaida
anakuwa ndani ya gari maalumu la limousine
au SUV. Alisema anakumbuka jinsi
alivyokuwa akijiendesha mwenyewe. “Napenda kuendesha,” alisema. “Hivi sasa
siwezi kuendesha tena.”
Vitu vingi juu ya Trump havijabadilika
kutoka usimamizi wa kibiashara na uandaaji vipindi vya televisheni akiendesha
mambo yake kutoka ghorofa ya 26 ya jengo la Trump Tower jijini New York huku
akitumia muda mwingi kwenye simu.
Amekuwa akiwasiliana na marafiki zake wa
nje na wabia wake wa kibiashara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine chanya.
Wasaidizi wake waandamizi wanasema wao wameachana na hali hiyo.
Rais huyo amekuwa katika mgongano na
mashirika mengi ya habari tangu kampeni zake za uchaguzi na kuamua kutohudhuria
Chakula cha Usiku cha Waandishi wa Habari wa Ikulu jijini Washington, D.C., kwa
sababu alihisi hakutendewa haki na vyombo vya habari.
“Nitakuja mwakani, kwa hakika,” Trump
alisema alipoombwa kama atahudhuria hafla hiyo siku zijazo.
Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na Chama
cha Waandishi wa Habari wa Ikulu. Mwandishi wa Reuters, Jeff Mason ndiye rais
wake.
0 comments:
Post a Comment