Joyce Kasiki, Dodoma
Marwa Chacha |
WATU watatu
akiwamo mama na watoto wake wawili, wamefariki dunia katika Jimbo la Serengeti mkoani
Mara baada ya kula mihogo iliyodhaniwa kuwa na sumu kufuatia ukosefu wa chakula
ubalikabili jimbo hilo.
Mbunge wa
Serengeti Marwa Chacha (Chadema) alibainisha kutokea kwa vifo hivyo jana wakati
akiomba mwongozo wa Spika, bungeni mjini Dodoma.
“Hali ni mbaya
watu wanakufa Serengeti. Katika Mkoa wote wa Mara, debe moja la mahindi
linauzwa kati ya Sh. 25,000 na Sh. 30,000” alisema Marwa.
Alisema hali
hiyo ya uhaba wa chakula pia imesababishwa na tembo ambao wamekuwa wakila mazao
ya wananchi kila yanapofikia wakati wa kuvunwa.
Alieleza kusikitishwa
na kitendo cha Serikali kushindwa kutoa chakula cha bei nafuu kwa wananchi
wakati katika baadhi ya maghala ya Serikali kuna chakula kimerundikana na
kinaoza wakati wananchi wanakufa kwa njaa.
"Tumeenda Shinyanga
kwenye ghala la Serikali, tumekuta mahindi yanaoza, lini mahindi hayo
yanatumika kama siyo wakati huwa njaa," alihoji Marwa
Katika mwongozo
wake aliliomba Bunge liache kujadili shughuli zilizopangwa kwa siku hiyo na
kujadili hoja yake ya uhaba wa chakula.
"Naomba
tuahirishe hoja, ili tujadili suala la njaa, sisi hatutaki chakula cha njaa, tunataka
chakula cha bei nafuu,"alisema.
Akijibu mwongozo
huo, Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson alivitaka vyombo vinavyohusika
kufuatilia suala hilo na kulipatia ufumbuzi huku akitaka chakulaki.ichopo
kwenye maghala kipelekwe kwa walengwa.
"Waziri wa
kilimo yupo hapa na Bunge lilishahakikishiwa kwamba chakula kipo na hayo
mahindi yanayooza yapelekewe kwa wahitaji," alisema Dk.Tulia
0 comments:
Post a Comment