Suleiman Msuya
BENKI nyingi nchini ziko hatarini
kushindwa kujiendesha kutokana na soko lake kutekwa na kampuni za simu za
mkononi.
Hayo yamo katika ripoti ya hali ya
uchumi nchini iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) juzi Dar es Salaam, ikionesha
kwamba asilimia 22 ya watumiaji wa simu wanahifadhi na kusambaza fedha kupitia vifaa
hivyo.
Ripoti hiyo ambayo imeanisha mambo
mbalimbali kuhusu hali ya uchumi nchini imebanisha kuwa kwa sasa benki
zinahifadhi asilimia nane ya fedha nchini.
Ilibanisha kuwa baada ya simu mfumo
unafuata kwa kutunza fedha ni majumbani kwa asilimia 21 hasa vijijini na benki
ikiwa asilimia nane.
Aidha, ripoti hiyo ya tisa kuhusu hali
ya uchumi inabainisha kuwa utaratibu mwingine ambao unatumiwa kuhifadhi fedha
ni kupitia familia, marafiki ambao ni asilimia mbili, Saccos asilimia moja na
MFI asilimia moja.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa benki na
taasisi zingine za fedha katika miaka ya nyuma, zilikuwa na watumiaji asilimia
11.9 ili kwa sasa wamefikia chini ya asilimia tisa hiyo ikionesha ishara kubwa
ya mtu mmoja mmoja kuhamia kwenye huduma za kifedha za simu.
Hali kadhalika mfumo wa kupokea au
kuweka fedha kupitia simu unaruhusu mteja kuweka hadi Sh milioni tatu ambapo
makato hayazidi asilimia mbili hadi tano tofauti na benki ambapo inafikia
asilimia 22.
Akizungumzia eneo hilo mmoja wa
waandaaji wa ripoti hiyo kutoka WB, Andrea Dall’Olio alisema mabadiliko hayo ya
matumizi ya simu kama njia ya kupokea na kutuma fedha, yanakuja kwa kasi kubwa
duniani kote hivyo kuhitajika mifumo sahihi ya kuratibu.
Dall’Olio alisema tangu mwaka 2013 hadi mwaka
juzi ongezeko la matumizi ya mitandao ya simu katika rika zote yamekuwa
yakiongezeka, hali ambayo inaenda kwa kasi kubwa.
“Uhifadhi fedha katika rika zote ni asilimia
44 kwa asilimia 61, na watumiaji walio hai kwa sasa ni asilimia 91 kwa 92 na
watumiaji wa huduma hizo ni asilimia 15 kwa 34,” alisema.
Aidha, akizungumzia hali ya ukopaji,
alisema ripoti imebaini kuwa asilimia 63 ya mikopo inapitia marafiki, familia na
majirani, kupitia simu ni asilimia 17, biashara za bidhaa asilimia 10, benki
asilimia saba na zingine nyingi.
0 comments:
Post a Comment