Grace Gurisha
Marehemu Sengodo Mvungi |
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam inatarajia
kusikiliza mashahidi 30 na kupitia vielelezo 13 ikiwemo bastola moja katika
kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo
Mvungi, baada ya watuhumiwa wa kesi hiyo kusomewa maelezo ya mashahidi.
Washtakiwa hao ni John Mayunga (56), Juma Kangungu (29),
Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo
(30) , Mianda Mlewa (40) na Msungwa Matonya (30) wote wakazi wa Dar es Salaam.
Washtakiwa hao walisomewa maelezo yao jana na Wakili wa
Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambapo katika maelezo hayo ya mashahidi
washtakiwa hao walikiri kutenda kosa hilo.
Mwita alidai kuwa katika kesi hiyo kutakuwa na mashahidi
30 na vielelezo 13 ikiwemo bastola, mapanga matano na hati ya ukamataji.
Baada ya washtakiwa hao kumaliza kusomewa maelezo hayo,
Hakimu Simba alisema washtakiwa hao watakaa mahabusu hadi tarehe ya kusikilizwa
kwa kesi hiyo itakapopangwa na Mahakama Kuu katika vikao vyake.
Awali, washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa 11 mmoja
akafariki wakabaki 10, ambapo kati hao Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP),
Biswalo Mganga liwasilisha mahakamani
nia ya kutokuendelea kuwashtaki washtakiwa wanne kwa hiyo wakabaki sita.
Washitakiwa hao walioachiwa huru baada ya kusota rumande
miaka minne ni Ahmed Kitabu (30), Zacharia Msese (33), Masunga Makenza (40) na
Msungwa.
Inadaiwa kuwa washtakiwa hao Novemba 3, mwaka 2013,
wakiwa eneo la Msakuzi Kiswegere
lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua
Dk Mvungi.
0 comments:
Post a Comment