Grace Gurisha
WAFANYABIASHARA
watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, akiwamo Ali Hatibu Haji ‘Shikuba’,
wanaendelea kusota rumande, wakisubiri rufaa waliyokata kupinga kuwekwa
kizuizini ipangiwe Jaji atakayeisikiliza.
Rufaa
hiyo iliwasilishwa juzi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na
mawakili wa washitakiwa hao, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo.
Akizungumza
kwa njia ya simu jana, Ndusyepo alisema waliwasilisha rufaa yao,
wanachokisubiri sasa ni namba ya rufaa hiyo na Jaji atakayeisikiliza, “hadi kesho
tutajua nini kinaendelea”.
Watuhumiwa
wengine ni Idd Mfuru na Tiko Emmanuel, ambao wote ni Watanzania.
Watuhumiwa
hao wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kukubali
maombi ya Waziri wa Sheria na Katiba ya kuwasafirisha Marekani kujibu tuhuma za
kujihusisha na dawa hizo.
Awali,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alikubali washitakiwa
hao wasafirishwe Marekani na pia aliamuru wakae rumande hadi Waziri wa Sheria
na Katiba atakapopata kibali cha kuwasafirisha.
Uamuzi
huo ulitolewa baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki kuwasilisha
maombi hayo.
Wakati
maombi hayo yanasikilizwa, Kakolaki alidai yameambatanishwa na hati ya kiapo
cha Wakili wa Serikali Msaidizi wa Texas, Richard Magnes ambacho
kilithibitishwa na kuapiwa kwa Jaji Nancy Johnson.
Kiapo
hicho kinaeleza jinsi watuhumiwa hao walivyoshiriki kwenye mashitaka hayo,
ambapo katika ushahidi ilidaiwa kuwa kuna mtu alipandikizwa kuchunguza
wanavyoingiza dawa hizo Marekani.
0 comments:
Post a Comment