Abraham Ntambara
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Dk James Jesse, ameishauri
Serikali kuwasilisha bungeni marekebisho ya Sheria ya Upigaji Kura ya Maoni ya Katiba
Mpya ili kuendelea na mchakato wake kwani imepitwa na wakati.
Alitoa
kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili ya
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Baraza la
Uongozi la Dini na Amani (IRCPT) akisema marekebisho hayo yatafanya mchakato huo
uende vizuri.
“Vifungu
namba nne na tano vya hiyo sheria vinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili mchakato
uanze upya, vimepitwa na wakati,” alisema Dk Jesse.
Alisema
maboresho hayo yanatakiwa kufanyika, kwani kwa sasa vifungu hivyo haviwezi
kutumika kutokana na kwamba tarehe iliyopangwa kupiga kura ilishapita, kadhalika
taratibu za kuendesha elimu ya mpiga kura haikufanyika.
Dk
Jesse alieleza kuwa kutokana na hali hiyo inatakiwa kutangazwa upya tarehe ya
kupiga kura ya maoni na kutoa muda kwa ajili ya elimu ya mpiga kura ili
wanaounga mkono Katiba pendekezwa na wanaopinga waelimishwe juu ya
wanachokiamini akisema baada ya hayo kufanyika ndipo kura ya maoni ifuate.
Alisema
kutokana na kutoshiriki kikamilifu kwa wapinzani wakati wa kuijadili bungeni,
Dk Jesse aliomba pia washirikishwe ili maoni yao mazuri yaongezwe kwa ajili ya
kuiboresha Katiba hiyo.
Mkurugenzi,
Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga alisema lengo la semina hiyo ni
kuwafundisha viongozi wa dini, ili waweze kushiriki kikamilifu katika suala la
kurudisha mchakato wa Katiba Mpya.
“LHRC
ina makubaliano na IRCPT kurudisha mchakato wa Katiba Mpya, tuna makubaliano ya
kufundisha viongozi wa dini ili wachukue nafasi yao kwa ajili ya mchakato wa Katiba,
ulianza na kuishia katikati,” alisema Henga.
Alisema
wanataka mchakato urudi ambapo inatakiwa makundi yaweze kuchukua nafasi katika kuishauri
Serikali.
Mkurugenzi
wa IRCPT, Thomas Godda alisema anatamani kile ambacho kilianza kifikie tamati,
kwani mchakato wa Katiba uligharimu fedha nyingi ambapo alieleza kuwa
angefurahi kama Katiba ingekamilika kabla ya 2020.
0 comments:
Post a Comment