Joyce Kasiki, Dodoma
Hifadhi ya Ngorongoro |
WIZARA ya
Maliasili na Utalii iko kwenye maandalizi ya awali ya kufanya marekebisho ya
sheria iliyoanzisha eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Ramo Makani alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Molel (CCM).
Katika swali
lake, Molel alitaka kujua ni lini Serikali itarekebisha sheria hiyo ya
mwaka 2002 ili wananchi wapate maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na
ufugaji.
Makani alisema
ni muhimu kuzingatia, kwamba katika marekebisho hayo, Serikali itaweka
msisitizo zaidi katika kuboresha shughuli za uhifadhi wa eneo la Ngorongoro ili
ibaki katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia.
Alikiri kuwa sheria
hiyo iliyotungwa mwaka 1959 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 inazuia
wananchi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kulima bali kufuga peke yake.
Hata hivyo,
alisema kabla ya mchakato huo utatanguliwa na shughuli za kitaalamu
ambapo ndani ya wiki moja kikosi cha sensa kwa watu Ngorongoro kitafanya
kazi ili marekebisho hayo yawe ya kisayansi.
"Wakati Mamlaka
hiyo inaanza ilikuwa na watu 8,000 lakini
hadi mwaka 2011 kulikuwa
na zaidi ya watu 89,000 , hivyo mabadiliko ya sheria hiyo yanatakiwa kuangalia
vitu mbalimbali ikiwamo idadi ya watu," alisema Makani.
Makani alisema
katika mwaka wa fedha ujao, mchakato wa sheria hiyo utaanza na kukamilika ndani
ya kipindi hicho.
Alisema kutokana
na zuio la kisheria la kulima, wakazi wa
Ngorongoro ambao
kwa asili ni wafugaji, wamekuwa
wakitengewa
bajeti ya kununulia mahindi ambapo takribani tani 3,600 hugawiwa bila malipo
kila mwaka kwa matumizi ya chakula hususan kwa wenye kipato ca chini na
wasiojiweza na kwa wenye uwezo huuziwa kwa bei nafuu.
"Ili kukabiliana
na changamoto ya chakula, mwaka 2007 Mamlaka ilianza mchakato wa kupata maeneo
ya kilimo
nje ya hifadhi
kwa kutenga bajeti na kuwezesha mradi wa JEMA katika kata ya Oldonyosambu, ukiwa
na lengo la kuondoa wahamiaji haramu walioingia ndani ya Hifadhi.
Pia alisema
malengo yalikuwa ni kutoa fursa kwa wenyeji halali ambao wangependa
kufanya shughuli za kilimo na ufugaji nje ya Hifadhi.
0 comments:
Post a Comment