Grace Gurisha
KESI ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili vigogo wawili
wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha ushahidi, baada ya
washitakiwa kusomewa maelezo yao ya awali.
Kesi hiyo namba 102 ya 2017 itasikilizwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, ambapo upande wa Jamhuri utawakilishwa na
mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru.)
Vigogo hao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Cosmas Mwaifwani
na Kaimu Meneja Ununuzi, Frederick Nicolaus, ambao waliposomewa maelezo hayo
walikubali majina yao na vyeo vyao, lakini wakakana tuhuma zinazowakabili.
Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Machi mosi na 19, 2013 wakiwa
makao makuu ya MSD Temeke, Dar es Salaam, kwa nafasi zao walitumia madaraka
vibaya kuandaa, kusaini mkataba namba
moja wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/1011/60
wa Machi mosi, 2013.
Pia wanadaiwa kuwa waliandaa waraka wa mwito namba 2 wenye
kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/2011/60 wa Machi 19, 2013 na kuisababishia kampuni
ya H.H. Hillal & Company Limited kupata manufaa ya Sh 482,266,000.
Baada ya kusomewa mashitaka, walikana na kuwa nje kwa
dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
0 comments:
Post a Comment