Mwandishi Wetu
Ali Hatibu Haji ‘Shikuba' |
WAFANYABIASHARA
watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, akiwamo maarufu Ali Hatibu
Haji ‘Shikuba’, wanatarajia kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar
es Salaam dhidi ya kuwekwa kizuizini kusubiri kupelekwa Marekani kushitakiwa.
Watuhumiwa
wengine ni Idd Mfuru na Tiko Emmanuel, ambao wote ni Watanzania, lakini
wanahitajika Marekani kutokana na tuhuma za biashara za dawa za kulevya
zinazowakabili.
Hatua
hiyo ilifikiwa na mawakili wa wafanyabiashara hao, Hudson Ndusyepo na Majura
Magafu, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kukubali maombi ya Waziri wa
Sheria na Katiba ya kuwasafirisha Marekani kujibu tuhuma za kujihusisha na dawa
hizo.
Akizungumza
kwa njia ya simu jana, Wakili Ndusyepo alisema lazima leo wakate rufaa Mahakama
Kuu, kupinga uamuzi huo kwa sababu tayari Mahakama ya Kisutu imekubali kusudio
lao la kukata rufaa, kwa hiyo wanachosubiri ni mwenendo wa maombi hayo.
“Tungekuwa
tumeshakata rufaa, lakini bado mwenendo wa kesi ulikuwa bado haujamalizwa
kuchapwa, kwa hiyo kesho (leo) watamalizia na siku hiyo hiyo tutakwenda
Mahakama Kuu kwa sababu wateja wetu wako mahabusu hivi sasa,” alisema Ndusyepo.
Awali,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alikubali washitakiwa
wasafirishwe Marekani na akaamuru wakae rumande hadi Waziri wa Sheria na Katiba
atakapopata kibali cha kuwasafirisha.
Uamuzi
huo ulitolewa baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki kuwasilisha maombi
hayo. Wakati maombi hayo yanasikilizwa, Kakolaki alidai kuwa yameambatanishwa
na hati ya kiapo cha Wakili wa Serikali Msaidizi wa Marekani Texas, Richard
Magnes ambacho kilithibitishwa na kuapwa kwa Jaji Nancy Johnson.
Kiapo
hicho kinaeleza watuhumiwa hao walivyoshiriki katika mashitaka hayo, ambapo
katika ushahidi, inaelezwa kuwa kuna mtu alikuwa amepandikizwa kuchunguza jinsi
wanavyoingiza dawa za kulevya Marekani.
0 comments:
Post a Comment