Grace Gurisha
Ali Hatibu Haji |
WAFANYABIASHARA
watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, akiwamo maarufu Ali Hatibu
Haji ‘Shikuba’, wanatarajia kukata rufaa leo Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Dar es Salaam, kupinga kuwekwa kizuizini kusubiri kupelekwa Marekani kushitakiwa.
Watuhumiwa
wengine ni Idd Mfuru na Tiko Emmanuel, wote ni Watanzania. Rufaa hiyo
inatarajiwa kuwasilishwa mahakamani hapo kupitia mawakili wao, Hudson Ndusyepo
na Majura Magafu.
Mawakili
hao walifikia hatua hiyo, baada ya kupata mwenendo wa maombi ya Marekani ya
kuwahitaji kutokana na tuhuma za biashara za dawa za kulevya zinazowakabili
nchini humo yaliyokuwa yakisikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
“Tutakata
rufaa leo Mahakama Kuu, kwa sababu tayari tumepata mwenendo wa maombi ya wateja
wetu, awali tulishindwa kufanya hivyo kwa kuwa yalikuwa bado hayajamalizwa
kuchapwa,” alisema Ndusyepo.
Watuhumiwa
hao wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, kukubali maombi ya Waziri wa Sheria
na Katiba ya kuwasafirisha Marekani kujibu tuhuma za kujihusisha na dawa hizo.
Awali,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alikubali washitakiwa
hao wasafirishwe Marekani na pia aliamuru wakae rumande hadi Waziri wa Sheria
na Katiba atakapopata kibali cha kuwasafirisha.
Uamuzi
huo, ulitolewa baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki kuwasilisha
maombi hayo. Wakati yanasikilizwa, Kakolaki alidai kuwa yameambatanishwa na
hati ya kiapo cha Wakili wa Serikali Msaidizi wa Texas, Richard Magnes ambacho
kilithibitishwa na kuapwa kwa Jaji Nancy Johnson.
Kiapo
hicho kinaeleza watuhumiwa hao walivyoshiriki katika mashitaka hayo, ambapo
katika ushahidi inadaiwa kuwa kuna mtu alipandikizwa kuchunguza jinsi walivyoingiza
dawa za kulevya nchini humo.
0 comments:
Post a Comment